Mwenyekiti wa Yanga, Yusuf Manji.
MECHI ya watani haiishi vituko baada ya Mwenyekiti wa Yanga, Yusuf Manji, kujikuta akipandwa na jazba na kumvaa kiongozi wa Kamati ya Utendaji ya Simba, Musley Al Rawah, akitaka wazichape kavukavu.
Manji alifanya hivyo mara tu baada ya kumalizika kwa mechi ya watani Simba dhidi ya Yanga huku Wekundu wa Msimbazi wakiwa wameshinda kwa bao 1-0 jana kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar.
Sakata hilo lilianzia kwenye lifti za uwanja huo na kuendelea hadi chini wakati Al Rawah alipoingia kwenye vyumba vya wachezaji wa Simba na Manji akataka kumfuata huko lakini walinzi wake na watu wengine wa usalama wakamzuia.
Awali, taarifa zilikuwa zinababaisha baada ya kueleza kwamba walitaka kuzichapa baada ya Al Rawah kumsukuma kwa makusudi mtoto wa Manji aitwaye Mehbub Ally mwenye umri wa miaka 12.

Championi Jumatatu lilimtafuta Manji kuhusiana na suala hilo, akasema: “Kweli nasikitika sana, nimepandwa na jazba na hapa niko Hospitali ya Aga Khan, mwanangu anafanyiwa uchunguzi, daktari amesema apigwe x ray.
“Tulikuwa kwenye lifti, yule bwana (Al Rawah), wakati mlango unafunga yeye akazuia, akaingia. Ikaonekana lifti imezidiwa, alitakiwa ashuke mtu, ajabu akamsukuma mwanangu nje.
“Kitendo hicho kilinishtua, kweli nikamsukuma ili nitoke kumfuata mwanangu nje ya lifti na pale tayari jazba zilinipanda. Huyu ni mtoto mwenye umri wa miaka 12 tu, vipi unaweza kumfanyia hivyo? Hapa si suala la mpira tena,” alisema Manji.
Alipotafutwa Al Rawah, alisema hakukuwa na tatizo kubwa na yeye wakati anashuka, alimgonga mtoto wa Manji.
“Alikuwa mbele yangu, sikujua hata ni mtoto wa nani. Nafikiri hakunielewa, hata nilipojaribu kutaka kumuelewesha, kutaka kumuomba msamaha, alionekana bado kuwa na jazba.
“Mwisho watu waliokuwa pale waliniondoa nikaendelea na shughuli za timu,” alisema Al Rawah. Hata hivyo, haikujulikana zaidi matokeo ya hospitali ya mtoto wa Manji yalikuwaje lakini Al Rawah aliendelea kusisitiza, kamwe hakuwa na nia mbaya kwa Manji wala mwanaye.
GPL
0 comments:
Post a Comment