KATIKA kile kinachoonekana kuwa ugomvi wao bado ni mbichi kabisa, nyota wa filamu Bongo, Wema Sepetu Jumanne wiki hii akiwa ni mshehereshaji katika sherehe ya kumbukumbu ya kuzaliwa kwa mtoto wa mtangazaji maarufu, Zamaradi Mketema, aligoma kumtaja Kajala Masanja kama mmoja wa watu waliotakiwa kula keki, Ijumaa lina mkanda kamili.
Nyota wa filamu Bongo, Wema Sepetu.
Kwenye sherehe hizo zilizofanyika nyumbani kwa mtangazaji huyo jijini Dar, baada ya mambo mengi kufanyika, ndipo ulipofika wakati wa mastaa kibao walioalikwa kuitwa majina yao kwa ajili ya kwenda kupewa keki katika meza kuu.
Mshangao mkubwa ulikuja wakati Wema, akitangaza kwa mbwembwe aliporuka kutaja jina la Kajala aliyekuwa akionekana dhahiri na kumtaja aliyemfuatia, jambo ambalo lilizua minong’ono kutoka kwa waalikwa wengine kiasi kwamba mmoja wao alichomoka na kwenda kumnong’oneza Wema juu ya kitu hicho na kumtaka akirekebishe.
Nyota wa filamu Bongo, Kajala Masanja.
“Jamani mtaniudhi sasa hivi, mimi siwezi kumtaja huyo mtu mbona mnanilazimisha nyie oooh,” Wema alisema kwa hasira kwa mtu huyo aliyelazimika kuondoka zake ili kuepusha shari.
Mastaa hao waliokuwa wamekaa meza moja lakini kila mmoja akiwa bize na mambo yake, waliwaumiza sana mastaa wenzao waliokuwa nao mezani kwani wote wanawapenda lakini wenyewe ndiyo hawapendani.
Kuona hivyo, Kajala ambaye pia alichelewa kuingia ukumbini kabla ya wenzake, aliamua kuondoka zake bila kusema chochote kuhusiana na suala hilo lililoacha simulizi kubwa.
0 comments:
Post a Comment