ZITTO Zuberi Kabwe
ZITTO Zuberi Kabwe ambaye ametangazwa na Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kwamba amevuliwa uanachama, anawatesa mashabiki wake kwa sababu hawajui atahamia chama gani.
Wakizungumza na Uwazi Mizengwe, baadhi ya wanachama wa Chadema ambao ni wafuasi wa mwanasiasa huyo kijana, walisema hatma ya Zitto hawaijui kwa kuwa amekuwa mgumu kutoa uamuzi.
“Tulitegemea akiwa Kigoma angesema yeye sasa atakuwa chama gani lakini tulishangazwa zaidi baada ya kumuona juzi (Jumatano) akichangia bungeni,” alisema Kijo Ndeku, mkazi wa Mwenge.
Aliongeza kuwa sasa wana Chadema ‘Zitto Team’, wameachwa njia panda kwa sababu hawajui bosi wao ana mpango gani kisiasa.
“Alipokuwa jimboni kwake Kigoma Kaskazini tulimsikia Zitto akisema kuwa atakuwa rais wa nchi hii na atagombea lakini hakusema atapata nafasi hiyo kupitia chama gani au ni mwaka gani,” alisema Ali Issa Ali aliyejitambulisha kuwa ni mwanachama wa Chadema anayeishi Morogoro.
Hata hivyo, Zitto alipohojiwa na kituo kimoja cha televisheni mwanzoni mwa wiki hii na kuulizwa sababu ya kutimuliwa Chadema huku akidaiwa kuwa ni msaliti, alisema:
“Unajua mtu anapokufukuza hukuchagulia jina baya, hata mbwa akifukuzwa utasikia watu wakisema huyo ni mbwa koko, hivyo basi ninachosema mimi ni kwamba siku zijazo haya yatajulikana.
“Unajua kuna wakati niliambiwa eti nimepewa shilingi bilioni mbili nikiwa Ujerumani, nikasema jamani iundwe kamati kuchunguza madai hayo na ukweli ukijulikana kama siyo kweli aliyezusha hilo achukuliwe hatua. Wakakataa.”
Hata hivyo Zitto alisema mpaka sasa yeye ni mbunge wa Chadema na ataendelea kuwatumikia wapiga kura wake mpaka hapo mambo yatakapowekwa sawa kisheria.

0 comments:
Post a Comment