Gari la kampuni ya magazeti ya Mwananchi limekamatwa na polisi mkoani Iringa kwa madai ya kusafirisha madawa ya kulevya aina ya mirungi kutokea Dar Es Salaam kwenda Mbeya.
Taarifa zimedai kuwa gari hilo limekuwa na kawaida ya kufanya biashara ya kufanya magendo kama ya vipodozi na mirungi kabla ya polisi kuweka mtego jana usiku.
Hata hivyo mtego huo umefanikiwa kulikamata gari hilo na magunia ya madawa hayo aina ya mirungi ambayo idadi yake bado kufahamika.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Iringa amesema taarifa kamili ataitoa hapo baadaye.
0 comments:
Post a Comment