2014-12-24

Kime Buma; Waliokuwa watumshi hifadhi ya Ngorongoro kizimbani.

Waliokuwa watumishi wa Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro akiwemo aliyekuwa Mhifadhi Mkuu wa Mamlaka hiyo ambaye sasa ni Mbunge wa Bunge Afrika Mashariki Bernard Mrunya wamepandishwa kizimbani katika mahakama ya Wilaya ya Karatu kujibu tuhuma mbalimbali zinazowakabili. 


Miongoni mwa tuhuma hizo ni matumizi mabaya ya madaraka wakati wakiwa watumishi katika mamlaka hiyo

Waliofikishwa mahakamani hapo ni washtakiwa watano ambao ni pamoja na Bernard Mrunya aliyekuwa Mhifadhi wa mamlaka hiyo ambapo kwa sasa ni Mbunge wa bunge la Afrika Mashariki Afrika Mashariki, Leornard Minzi mkuu wa kitengo cha manunuzi pamoja na Victor Appolo ambae alikuwa alikuwa Mkuu wa Idara ya Ikolojia

Wengine ambao mpaka sasa ni watumishi katika mamlaka hiyo ni Bruno Kawasange Mkurugenzi wa hifadhi na maendeleo ya Jamii pamoja na Justice Muumba ambae ni Meneja wa maendeleo ya Jamii 


Akisoma hati ya mashtaka mbele ya Hakimu mfawidhi wa mahakama ya Wiolaya Ally Mkama mwendesha mashtaka wa Takukuru Hamidu Sindano waliieleza mahakama kuwa kwa tarehe tofauti kati ya mwezi Aprili na Februari 2011 na 2012 washtakiwa tajwa katika nafasi zao walitumia madaraka yao vibaya kwa kushawishi kumpa kazi mtaalamu mshauri Michel Duplat ambae ni mfaransa bila kufuata taratibu zilizoelekezwa na sheria za manunuzi ya Umma ya mwaka 2004 kitendo kilichopelekea Duplat kulipwa fedha za Umma kinyume na taratibu

Bwana Sindano alifafanua kuwa washtakiwa pia wanakabiliwa na makosa ya matumizi mabaya ya madaraka kinyume na kifungu cha 31 cha sheria ya kuzuia ya kuzuia na kupambana na rushwa no 11 ya mwaka 2007 na kuisababishia serikali hasara ya dolla za Kimarekani elfu 27.

Washtakiwa kwa pamoja hawakutakiwa kuzungumza chochote mahakamani hapo ambapo wameachiwa kwa dhamana kwa masharti ya kila mmoja kuwa na wadhamini wawili ambao watasaini hundi ya sh.ml 10 na kila mmoja kuwa na mali isiyohamishika ya dhamani ya sh.ml 10 pamoja na kutoruhusiwa kusafiri nje ya nchi ambapo kesi hiyo itatajwa tena Januari 06 2015.

0 comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...