Oohoo! Wakati staa mkubwa wa muziki wa Afro-Pop, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’ akichekelea kitendo cha mpenzi wake wa sasa, Zarinah Hassan ‘Zari’ au ‘The Boss Lady’ kunasa mimba yake, habari ya mjini huko Kampala, Uganda ni juu ya aliyekuwa mume wa mwanamama huyo, Ivan Ssemwanga kufunguka na kusema: “Naapa Zari hawezi kuzaa na Diamond.”
Staa mkubwa wa muziki wa Afro-Pop, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’ akiwa na Zarinah Hassan, 'Zari'.
HABARI YA MJINI
Wikiendi iliyopita, vyombo vya habari na mitandao nchini Uganda ambako kuna makazi mengine ya Zari mbali na Afrika Kusini, kulipambwa na habari hizo baada ya mwanaume huyo aliyezaa na mwanamama huyo watoto watatu kuanika siri nzito juu ya ishu hiyo.
‘Ubuyu’ huo ulidadavua kwamba, kwanza jamaa huyo mwenye utajiri wa kutupwa alianza kwa kuelezea namna alivyoshtuka aliposikia Zari ni mjamzito.
ASHANGAA KUSIKIA ZARI MJAMZITO
Alisema kwamba alishangaa kusikia Zari ni mjamzito wakati ana umri wa karibia miaka 40 na watoto watatu ambao amekuwa akiwapuuza na kuendelea kuzurura na mpenzi wake mpya, Diamond sehemu mbalimbali ndani na nje ya Bara la Afrika.
Ilielezwa kwamba Ivan aliweka wazi kuwa amekuwa na hofu kwa kuwa Zari ni mwanamke ambaye umri umemtupa mkono hivyo anaweza akashindwa na ‘stresi’ za malezi ya mtoto mchanga.
Maoni ya Ivan ameyatoa baada ya Diamond kufichua kwamba Zari ni mjamzito huku akitupia vielelezo vya vipimo mitandaoni vikionesha kiumbe anayekua tumboni kwa mwanamke, jambo lililosababisha jamii kuamini kuwa ni Zari kwa kuwa wawili hao wamekuwa wakionekana kimahaba na kulala chumba kimoja kwenye hoteli mbalimbali.
Jamaa huyo alisema yeye ameshazaa na Zari watoto watatu na kwa pamoja walikubaliana kwamba Zari asilete kiumbe mwingine duniani.
NI AJABU?
Kwa mujibu wa Ivan, aligundua kwamba Zari hawezi kuwatunza vizuri watoto wake hivyo ni ajabu kuona anaongeza mwingine.
“Kwa ninavyomjua Zari, naapa hawezi kuzaa na Diamond,” alikaririwa jamaa huyo bila kufafanua kama mimba ambayo tayari Zari anayo itakwenda wapi.
Watoto wa Ivan Ssemwanga na 'Zari'.
UMRI WA MWISHO KUZAA NI UPI?
Kutokana na maelezo ya Ivan, Ijumaa Wikienda liliingia mzigo kutaka kujua umri wa mwisho wa mwanamke kuzaa ni upi?
Kwa mujibu wa mtaalamu wetu, umri wa miaka 41 bado mwanamke ana uwezo wa kushika mimba kama hana matatizo yoyote ya kiafya ambayo yanaweza kuzuia kwa namna moja au nyingine asishike mimba.
Mara nyingi muda hasa wa mwisho kabisa ni umri wa miaka 45 endapo pia mwanamke anakuwa hana tatizo la kiafya.
Hata hivyo, umri mzuri wa mwisho wa kuzaa kwa mwanamke unaoshauriwa ni miaka 40 kwani nyonga zinakuwa zimeanza kuchoka hasa kama mama atakuwa amezaa kabla.
TURUDI KWA ZARI
Kwa maelezo ya mtaalam wetu, hata kama mwanamama huyo anakaribia umri wa miaka 40 si kigezo cha kushindwa kumzalia Diamond hivyo kinachohitajika ni uangalizi wa hali ya juu.
0 comments:
Post a Comment