Kamanda wa polisi mkoa wa Kigoma ACP Jafari Mohamed amesema, risasi 524 na bunduki moja ya kivita aina ya SMG zimekamatwa katika eneo la kijiji cha Nduta baada ya polisi katika kizuizi cha Nduta kufanya ukaguzi ndani ya basi.
Wakati kazi hiyo ikiendelea mtu anayesadikiwa kumiliki begi lililokuwa na risasi na bunduki alitoroka, ambapo amesema vizuizi vya barabarani vilivyowekwa katika maeneo mbalimbali mkoani Kigoma vimesaidia kukamata wahalifu na silaha zinazosafirishwa mara kwa mara.
Pia ametumia fursa hiyo kuishukuru serikali wilayani Kibondo kwa kutoa pikipiki tatu kwa jeshi la polisi.
Kwa upande wake aliyekuwa mkuu wa wilaya ya Kibondo Venance Mwamoto, ambaye amehamishiwa wilaya ya Kaliua mkoani Tabora, amewataka wananchi kutoa ushirikiano na kuisadia serikali kuimarisha ulinzi kwa kuwa jukumu la ulinzi ni la wananchi wote.
0 comments:
Post a Comment