Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC), Zitto Kabwe.
Pia yumo Bosi TRA, kufika mbele ya Kamati ya PAC, Zitto asema fedha hizo zipo za watu binafsi, kampuni.
Mbivu au mbichi za vigogo 99 wa Tanzania waliotajwa kuficha mabilioni ya fedha kwenye akaunti za siri nchini Uswiss zitajulikana hivi karibuni, Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC), Zitto Kabwe, amesema.
Kwa mujibu wa Zitto, PAC imewaita Gavana wa Benki Kuu (BoT), Prof. Benno Ndulu; Mwanasheria Mkuu wa Serikali (AG), George Masaju na Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Dk. Rished Bade, ili kuhojiwa na kamati yake Machi 9, mwaka huu. Akizungumza na NIPASHE jana jijini Dar es Salaam, Zitto alisema majina ya watu au kampuni zinazohusika na mabilioni hayo vitajulikana kwa kuwa serikali imeshachunguza na ripoti iko tayari.
0 comments:
Post a Comment