Watanzania wametakiwa kutembelea kutembelea (kutalii) kwenye mapango ya Amboni yaliyopo nje kidogo ya mji wa Tanga,kwani idadi imepungua kutokana na vyombo vya habari hasa magazeti kupotosha kuwa matukio ya kigaidi yaliyotokea hivi karibuni yalitokea maeneo hayo ya mapango.
Muongozaji wa Watalii katika mapango hayo aliyejulikana kwa jina la Bw.Tabu akizungumza na mtangazaji wa kipindi cha Power Breakfast cha Clouds FM,Saidi Bonge alipotembelea katika mapango hayo alisema kuwa tangu magazeti yalipotoa habari za upotoshaji kuwa mapigano ya magaidi na wanajeshi yalitokea katika mapango hayo watalii wamekuwa hawaendi tena kutembelea katika mapango hayo.
‘’ujue waandishi hawakufanya utafiti na waliandika habari si za kweli yale mapambano hayakutokea kwenye mapango ya Amboni ambayo watalii walikuwa wakija kutalii yalitokea kilomita sita kutoka kwenye mapambano hayo na sasa hivi serikali imekosa mapato kutokana upotoshaji huo,’’alisema Bw.Tabu.
Aidha aliongeza kuwa wanatarajia kufanya kampeni ili watu waende kutembelea mapango hayo na kwamba amewataka watalii wa ndani na nje wasiogope kutembelea kwani sehemu hiyo ni salama tofauti na taarifa zilivyotangazwa na vyombo vya habari.
0 comments:
Post a Comment