Francis Cheka
Cheka, leo Jumamosi anatimiza siku ya ishirini tangu awe gerezani kutokana na kifungo cha miaka mitatu baada ya kupatikana na hatia ya shambulio la kudhuru mwili dhidi ya meneja wa baa yake, Bahati Kibanda, lililofanyika Julai 2, mwaka jana.
Francis Cheka akiwa kwenye gari la polisi.
Akizungumza na Championi Jumamosi, Ustaadh alisema imemlazimu kuvunja kamati hiyo ya watu sita kwa kuwa wengi wao hawakuwa wakweli na walikuwa wanatafuta umaarufu kupitia jina la bondia huyo.
“Unajua tulipokuwa Morogoro, tuliunda kamati ambayo ilikuwa na watu sita kwa ajili ya kushughulikia suala la rufaa ya Cheka lakini nimegundua wengi wao siyo wakweli na wapo kwa ajili ya kutafuta umaarufu kupitia Cheka, sasa haitawezekana.
“Kutokana na hali hiyo, nimeunda kamati nyingine mpya inayoongozwa na mimi mwenyewe akiwemo Juma Msangi, Cosmas Cheka ambao naamini tutafanikiwa kwa sababu kila kitu kinaenda vizuri kama tulivyotarajia, kwani ukimya wetu unamaana kubwa sana,” alisema Ustaadh.
GPL
0 comments:
Post a Comment