Nyota wa filamu Bongo, Chuchu Hans ameibuka na kusema rafiki yake wa kiume, Vincet Kigosi ‘Ray’ amewakimbiza marafiki zake wote kwani tangu waanze uhusiano wao, hawapo karibu naye kwa vile awali walikuwa michepuko yake.
Nyota wa filamu Bongo, Vincet Kigosi ‘Ray’ akiwa na mpenz wake Chuchu Hans.
Akizungumza na Risasi Mchanganyiko hivi karibuni, Chuchu alisema baada ya mashostito hao kumkimbia alijiuliza sababu na alipochunguza akagundua kuwa wengi walikuwa wanajihusisha kimapenzi na Ray, ambaye pia ni muigizaji nyota.
“Unajua nilikuwa najiuliza sana kwa nini marafiki walitawanyika ghafla baada ya kuwa na uhusiano na Ray, nikagundua kuwa wengi wao walikuwa ni wake wenza ndiyo maana waliamua kujinasua wenyewe lakini nashukuru maisha yanaendelea,” alisema Chuchu.
0 comments:
Post a Comment