MREMBO anayekimbiza na ngoma ya Ulithemba, Esterlina Sanga ‘Linah’, juzikati alifunguka kwamba, wivu wa mchumba wake Nangari Kombo ‘Nanga’, nusura umkoseshe mamilioni ya fedha alizopewa kwenye udhamini na Kampuni ya Serengeti.Msanii wa muziki wa bongo fleva, Esterlina Sanga maarufu kama ‘Linah’.
Akiteta na paparazi wetu ndani ya Ukumbi wa Escape One, Mikocheni jijini Dar es Salaam hivi karibuni, alisema katika maisha yake ya kimapenzi amejifunza jambo muhimu sana la kupunguza wivu kwani ukizidi sana unaweza kumsababishia mtu kukosa vitu vya maana kwenye maisha.
“Nimeamini wivu ni adui mkubwa wa maendeleo kwenye maisha maana kama usipoweza kuuzuia unaweza kujikuta ukishindwa kutimiza ndoto zako kama ilivyotaka kunitokea kwani kila mara nilipokuwa nikiongea na bosi wa Serengeti mchumba wangu alikuwa akinikoromea hivyo kama ningemsikiliza nisingepata hili dili,” alisema Linah.
0 comments:
Post a Comment