Diamond Platnumz amepata shavu lingine la kutumbuiza kwenye sherehe za utoaji wa tuzo za ‘Africa Magic Viewers’ Choice Awards’ (AMVCA 2015), zitakazofanyika Jumamosi hii huko Lagos, Nigeria na kurushwa Live kupitia DSTV.
“Waliwasiliana na sisi kwa e-mail, na show itakuwa ni siku ya Jumamosi Tarehe 7,” amesema mmoja wa mameneja wake, Salaam kupitia 255 ya XXL ya Clouds Fm.
“Itakuwa ni live katika channel moja ya Africa Magic. Hizi ni tuzo za Afrika Magic movie awards ambazo zinafanyikaga Lagos, Nigeria, kwahiyo Diamond ataperform nyimbo ya Mdogomdogo…”
Ameongeza kuwa Diamond anaweza kufanya video ya wimbo wa Iyanya akiwa Nigeria.
“Msanii mwingine atakaye perform ni Iyanya ndo ambaye meneja wake niliongea naye kwasababu wanataka kushoot video na Diamond vilevile kwahiyo kulekule katika nyimbo yake ndo alituambia kuwa naye ana perform.”
0 comments:
Post a Comment