2015-03-13

RAY C AANZA TENA KUONESHA MAMBO YAKE


Ray C a.k.a Kiuno bila mfupaMsanii wa muziki wa kizazi kipya, Rehema Chalamila ‘Ray C,’ amesema ameanza kurejesha mwili wake wa zamani baada ya kufanya mazoezi kwa muda.

Ray C alikuwa hodari wa kunengua akiwa jukwaani, mashabiki walimpachika jina la ‘Kiuno bila mfupa.’ Akizungumza jijini, Ray C alisema ameridhia kurudisha mwili wake wa zamani, anafanya mazoezi huku akibadili matumizi ya chakula.

“Safari ya kupunguza mwili bado inaendelea, nashukuru nimeanza kuona mabadiliko, si rahisi ila nimezoea kupambana na lolote mbele yangu, nina uhakika nitashinda na hili. 


“Nafanya hivi kwa ajili ya mashabiki wangu wote nchini ili niweze kuwapa ladha kwa mara nyingine tena,”alisema

0 comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...