2015-01-31
Tunakufukulia kisa kilichomkuta mtalaka wa Isha Mashauzi!!!!!!!! TUNAFUKUA, Tufukue....
Mfanyabiashara, Jumanne Hassan ‘Tevez’ akiwa amefungwa kamba na watesi wake.
Januari 28, mwaka huu, picha za Tevez akiwa ametoka kuteswa kwa kudhalilishwa zilisambaa kwenye mitandao mbalimbali ya kijamii huku wengine wakidai kisa ni kukutwa na mke wa mtu, wengine wakisema ni dhuluma.
RISASI LAINGIA MTAANI KUCHIMBA
Risasi Jumamosi halikufanya haraka kuichapisha habari hiyo mpaka kuichimba kwanza ili kujua kisa na mkasa kamili ndipo iwapelekee wasomaji wake. Na ndivyo ilivyofanyika!
ENEO LA TUKIO
Risasi Jumamosi lilichimba na kubaini kuwa, tukio la Tevez kufanyiwa ukatili huo lilitokea kwenye mji wa Durban nchini Afrika Kusini ambako alikwenda kibiashara.
“Tukio si la Dar kama wanavyosema wengine, limetokea mjini Durban, Afrika Kusini. Si unajua jamaa (Tevez) ni mtu wa tripu za kibiashara!” alisema mtoa habari mmoja akiomba hifadhi ya jina lake.
Jeraha likiwa mgongoni mwa Jumanne Hassan ‘Tevez’ baada ya kuteswa.
WALIOFANYA UKATILI
Kwa mujibu wa chanzo hicho, watu waliomtenda Tevez ni jamaa zake anaofanya nao biashara ambayo Risasi Jumamosi halijaijua vizuri (ingawa kwenye mitandao ya kijamii wanadai ni madawa ya kulevya).
YATAJWA DHULUMA
Chanzo kikaanza kuanika historia nzima tangu Tevez hajafanyiwa utekaji na udhalilishwaji huo.
“Siku za nyuma Tevez alipewa mzigo nchini Tanzania ili awapelekee hao jamaa wa Afrika Kusini. Aliondoka jijini Dar kwenda Nairobi, Kenya kwa basi akiwa na begi.
“Alipofika Nairobi, ilidaiwa begi hilo alilisahau kwenye basi lakini wengine wanasema aliuuza Nairobi na kwenda Afrika Kusini akiwa na begi feki.”
TEVEZ AWASILI AFRIKA KUSINI, AKUMBANA NA MSALA
Habari zaidi zikachimbuka na kudai kwamba, Tevez aliwasili mjini Durban na kukutana na jamaa zake ambapo aliwaambia mzigo aliusahau kwenye basi.
“Kumbe inasemekana jamaa aliyemuuzia mzigo Nairobi anafahamiana na jamaa wa Sauz na aliwapigia simu kuwaambia kwamba, ameuziwa mzigo na Tevez.
“Kwa hiyo mpaka Tevez anawasili kule, jamaa walikuwa wanajua hana mzigo kwa kuwa aliuuza Nairobi,” kilisema chanzo.
‘Tevez’ akiwa na moja ya wadau wenzake katika biashara anazofanya huko Durban.
ATEKWA, ADHALILISHWA
Ikaendelea kudaiwa kuwa, madai ya Tevez yaliwakera jamaa kwa vile walijua kila kitu, hivyo walimteka na kuanza kumtesa kwa kumvua nguo zote, wakamfunga kamba za manila za rangi ya bluu na kuanza kumtesa kwa adhabu mbalimbali ili kumkomesha.
Inadaiwa katika adhabu hiyo, jamaa hao walimpiga na kitu chenye ncha kali hali iliyosababisha Tevez atokwe na damu na ngozi kuchubuka eneo la mgongoni.
MADAI WAKATI WA UDHALILISHWAJI
Inadaiwa wakati udhalilishaji huo ukiendelea, jamaa hao walikuwa wakisema wanachotaka ni mzigo wao na si kitu kingine.
MARAFIKI, JAMAA WA DAR
Kufuatia kusambaa kwa picha hizo mtandaoni, marafiki na jamaa wa Tevez waliopo Bongo walilazimika kufanya mpango kwa kuwasiliana na watu wa karibu waliopo Durban kumnusuru Tevez kwa kumpeleka hospitali ambako anapata matibabu hadi juzi, Alhamisi.
Risasi Jumamosi: “Kuna habari alikatwa sehemu za siri ni kweli?”
Chanzo: “Si kweli.”
Risasi Jumamosi: “Inasemekana alifanyiwa kitu mbaya cha mambo ya Sodama, ni kweli?”
“Si kweli. Watu wanasema tu. Ila walimtesa sana kwa kweli.”
Bw. Jumanne Hassan ‘Tevez’ akiwa na moja ya jamaa zake sauzi.
RISASI LATINGA DUKANI KWA MKEWE WA SASA
Ili kuzidi kupata habari zaidi, Januari 28, mwaka huu, usiku Risasi Jumamosi lilikwenda Kinondoni Kwamanyanya, Dar kwenye duka la mke wa sasa wa Tevez ili kumsikia anasema nini kuhusu tukio hilo.
Paparazi wetu hakumkuta mke huyo lakini alibahatika kuongea na msichana aliyekuwa nje ya duka hilo na kumuuliza aliko Tevez.
Msichana: “Tevez yupo safarini Morogoro.”
Risasi Jumamosi: “Mbona hapatikani hewani? Nipe namba zake nyingine.”
Msichana: “Nilizonazo ndiyo hizohizo ulizonazo wewe, ni…(akazitaja).”
Kweli namba hizo ndiyo alizokuwa nazo paparazi wetu.
MAMA MKWE WA TEVEZ
Kesho yake, Risasi Jumamosi lilimsaka kwa simu mama mkwe wa zamani wa Tevez (mama wa Isha) lengo ni lilelile, kutaka kujua kama naye ana taarifa hizo na anasemaje.
“Ni kweli nimesikia na nimeona picha zake yaani nimesikitika sana kiasi kwamba nikawa siamini kama ni kweli yeye anaweza kufanyiwa ukatili wa aina hiyo.
“Kikubwa namshukuru Mungu kusikia yupo hai na kwa maana hiyo namuombea zaidi ili arudi katika afya yake,” alisema mama mkwe huyo aitwaye Rukia Juma.
Bw. Jumanne Hassan ‘Tevez’akiwa na mkewe.
MTU WA KARIBU NA TEVEZ
Risasi Jumamosi liliendelea kutafuta undani zaidi wa tukio la Tevez kwa kuongea na watu wake wa karibu waliopo Durban, ndipo likapenyezewa ishu mpya kuwa, baadhi ya ndugu na wafanyabiashara wenzake na Tevez wamechanga na kurudisha mali zilizokuwa zikidaiwa na jamaa hao.
“Nilikuwa Durban muda si mrefu na hapa ndiyo narejea nyumbani (Bongo). Kiukweli tukio la Tevez ndiyo habari ya mjini Sauz, maana jamaa wamemfanyia mbaya kinoma lakini kusema kweli hajakatwa nyeti kama mitandao ya kijamii inavyoandika, wamempiga sana.”
“Kingine ambacho ninajua tayari ameshatolewa kwenye jengo alilokuwa ametekewa na sasa yupo hospitali maalum ambayo siwezi kukutajia, ila huenda hali yake ikawa nzuri kama kweli atakuwa chini ya uangalizi wa madaktari,” alisema jamaa huyo.
Source:GPL
ALICHO SEMA DIAMOND KUHUSU EX WA ZARI
Stori: Musa Mateja/Risasi
ICON wa Bongo Fleva Nasibu Abdul ‘Diamond’, juzikati aliamua kumtolea uvivu, aliyewahi kuwa mpenzi wa mwandani wake wa sasa, Zarinah Hassani ‘Zari’,
King lawrenc kwa kumuita mpuuzi anayetafuta kiki kwa vile kila kukicha kazi yake ni kumfuatafuata kwa maneno ya kejeli na kumtusi.
Mke wa mtu sumu!!!!! yamtokea puani muuza genge
Stori: Dustan shekidele. Morogoro/Risasi
Aibu kubwa! Muuza genge mmoja kwenye Soko la Mji Mpya mjini hapa ambaye jina halikupatikana mara moja, amejikuta akichezea kichapo kwa madai ya kunaswa na mke wa mtu kisha kutembezwa mtupu mtaani.
Muuza genge aliyechezea kichapo baada ya kunaswa na mke wa mtu na kutembezwa mtupu mtaani.
Fumanizi hilo lililojaza umati wa jinsi na rika zote wakiwemo watoto lilijiri katikati ya wiki hii, maeneo ya Mji Mpya ndani ya chumba na kitanda cha wanandoa hao.
Kikiwa kwenye mishe zake, kile kikosi kazi cha Oparesheni Fichua Maovu (OFM) cha Global Publishers mkoani hapa kilipenyezewa kuwepo kwa ‘uovu’ huo ambapo hakikulaza damu.
ENEO LA TUKIO
OFM, ikiwa eneo la tukio ilijikusanyia madai mazito juu ya jamaa huyo kuwa amekuwa na kasumba ya kumhonga vyakula mke huyo wa mtu ambaye naye kwa kukosa uaminifu kwenye ndoa alijikuta akiingia mkenge hasa mumewe anapokuwa safarini kwa kuwa ni mtu wa kusafiri katika biashara zake binafsi.
Ilidaiwa kwamba, mwanamke huyo hutumia mwanya huo kumwingiza mchepuko wake huyo kwenye chumba na kitanda anacholala na mumewe kisha ‘kufanya yao’.
Baada ya kukolea huku mahaba niue yakitajwa na sauti ‘tamutamu’ zikisikika chumbani, majirani walikerwa na kitendo hicho cha jirani yao kudhulumiwa ‘mali’ zake ndipo wakaamua kumpa ‘ubuyu’ mume.
Ilisemekana kwamba, mume, akishirikiana na majirani aliowaomba ushirikiano, aliweka mtego ambapo alijifanya anasafiri kama kawaida.
Siku ya tukio, saa husika ilifika, kama kawaida jamaa alifika nyumbani kwa wanandoa hao kisha kuchoma chumbani kwa wanandoa tayari kwa kulicheza ‘segere’.
LAIVU NA SUTI YA KUZALIWA
Mwenye mke, akiwa chimbo alitonywa na majirani kuwa mambo ‘yamekwiva’ chumbani ndipo akawaibukia na kumkuta jamaa laivu akiwa mtupu. Haikujulikana kama ilikuwa ‘tayari au bado’.
Akiwa na hasira, mwenye mke alidaiwa kumshushia kipigo mgoni kilichomfanya kuloa damu chapachapa na baadaye kumtoa nje akiwa mtupu kisha kumtembeza mtaani kwenda nyumbani kwake huku ‘kadamnasi’ ikipiga kelele ‘watu weweee...”
Katika hali ya kushangaza, mwenye mke aliomba mkewe asipigwe picha akidai bado anampenda na hayuko tayari kumuacha.
Kwa upande wake, jamaa huyo aliyedaiwa kufumaniwa alipohojiwa na OFM, aligoma kuzungumza na badala yake alificha uso kwa aibu.
Lily Carazona sasa ni nooma, aamua kuipasua intanet!! Kama una roho ndogo usibofye utapasua moyo wako
Mwanasheria mbichi kabisa ametikisa milango ya mageti ya intaneti kwa vitendo vyake ambavyo havitatoka kwenye kuta za mioyo yetu kwa urahisi. Ni kweli nakuambia
Shabiki mmoja alisema "I will not go to lengths to try and describe just how good she is at staying on the top of her game, but for a PR move this is the best she has posted yet , and the girl is on trail of making a mark on all levels of "socialite-dom" only a few days ago she posted a mega hip-swaying video of herself sporting the tightest body con ever"
Hivyi ndivyo alivyovunja mageti ya mtandao



Siku chache baada ya Shilole Kiuno, kumpiga Nuh. Wanaswa na camera wakivinjari kiivi
Siku chache baada ya Shilole kumzaba makofi Nuh mbele ya kadamnasi ambapo wahsabiki wake hawakufaurahishwa na jambo hilo kwenye instagram, Shilole ameamua kuomba msamaha kwa mpenzi wake na washabiki wake.
"Hii ni kwa mashabiki wangu wote nawapenda sana pili! Nawaomba radhi kwa kitendo kilichotokea juzi binafs sikupenda but ni hasira tu. Mm pia ni binaadam so kukosea ni kawaida so pili nimuombe na mpenzi wangu kwa nilichofanya! Nawapenda sana haitojitokeza tena one love sana" Shilole
Inaonyesha wawili hao wameweka tofauti zao pembeni na kuyamaliza
2015-01-30
Shocking: Suge Knight afanya mauaji, akamatwa
Suge Knight
Polisi nchini Los Angeles inasema kuwa msanii wa muziki wa rap kutoka Marekani Marion Suge Knight amekamatwa kutokana na mashtaka ya mauaji baada ya kumgonga mtu mmoja na gari lake hadi kumuua na baadaye kutoroka.
Polisi wanasema kuwa bwana Knight alijibizana na watu wawili katika eneo la kuegesha magari na baadaye kumgonga mmoja wao huku mwengine akijeruhiwa vibaya.
Wakili wake anasema ilikuwa ajali na kudai kuwa mteja wake alishambuliwa na watu wawili.
Suge Knight ni mwanzilishi wa kampuni ya Death Row Records ambayo iliwazindua wasanii maarufu wa mziki wa rap akiwemo Snoop Dogg na marehemu Tupac Shakur.
PICHAZ: Wafuasi wa CUF wapata dhamana
WAFUASI 29 kati ya 30 wa CUF waliokamatwa kwenye jaribio la maandamano ya kuwakumbuka wafuasi wenzao waliouawa mwaka 2001, Mbagala-Zakhem jijini Dar sanjari na mwenyekiti wao, Prof. Ibrahim Lipumba, mchana huu wameachiwa kwa dhamana katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu.
Wafuasi hao wameachiwa leo kwa dhamana baada mwenyekiti wao kupandishwa kizimbani juzi katika Mahakama Kisutu kujibu kesi ya kuhamisisha wafuasi wa chama hicho kutenda kosa la jinai kuhamasisha maandamano Januari 27, mwaka huu.
Wafuasi hao 29 walikidhi vigezo vya udhamini na kuachiwa lakini mwenzao mmoja ambaye aliendelea kushikiliwa hadi pale baada ya mdhamini wake kuchelewa kutimiza masharti ya dhamana.
Hakimu Mkazi, Emilius Mchauru alisema shauri hilo litasikikilizwa tena Februari 12, mwaka huu.
gpl
Upangaji wa matokeo, sasa ngoma nzito FIFA watua kuingilia sakata
Ujumbe maalumu wa Shirikisho la Soka la Kimataifa (Fifa) umetua nchini kwa siri kuchunguza tuhuma za upangaji matokeo unaowakabili waamuzi watatu waliosimamishwa tangu mwaka jana.
Waamuzi hao, Jesse Erasmos, Hamis Chang’walu na Oden Mbaga ambao awali walikuwa na beji ya Fifa, walisimamishwa kwa tuhuma ambazo hazijawekwa wazi.
Julai 24 mwaka jana, Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Jamal Malinzi alitangaza kuwasimamisha waamuzi hao kwa tuhuma za kupanga matokeo, ambazo hakuziweka wazi.
“Waamuzi hao waliosimamishwa na TFF pamoja na watu wengine watahojiwa na ujumbe huo wa Fifa na matokeo ya uchunguzi huo, yatatangazwa na Fifa wenyewe baada ya shughuli hiyo kukamilika,” alisema Mkurugenzi wa Mashindano wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Boniface Wambura.
“Tunaendelea kuwahimiza wanafamilia wa mpira wa miguu nchini wazidi kuzingatia kanuni za maadili za TFF, Shirikisho la Mpira wa Miguu Afrika (CAF) na zile za Fifa katika utendaji wao. Fifa kwa upande wake itahakikisha kuwa haki inatendeka katika uchunguzi ambao inaufanya,” alisema.
Hata hivyo, akifafanua suala hilo, Katibu Mkuu wa TFF, Celestine Mwesigwa alisema: “Mwaka jana tulipokea barua ya Fifa ikitutaka kuwasimamisha waamuzi hao na kwamba wapo kwenye uchunguzi, sasa huo uchunguzi hatutajua unahusisha mechi za ndani au za nje za kimataifa au zote kwa pamoja.
“Sisi (TFF) tumewaandalia sehemu maalumu watakayofanyia shughuli yao, lakini hakuna kiongozi yeyote anayeruhusiwa kusikiliza hadi uchunguzi wao utakapokamilika, ndiyo watatuletea,” alieleza Mwesigwa.
SWALI: Ujumbe maalum uliokuja kuchunguza sakata la upangaji matokeo umetokea wapi?
a. FIFA
b. Kenya
c. Njombe
Kushiriki kujibu swali hili na ushinde na pia uwe mfukuaji bora bofya hapa
MUGABE awa mwenyekiti mpya AU
Rais Robert Mugabe wa Zimbabwe ndio mwenyekiti mpya wa Umoja wa Afrika -Au
Rais mkongwe wa Zimbabwe Robert Mugabe, mwenye umri wa miaka tisini, sasa ameteuliwa kuwa mwenyekiti wa muungano wa Afrika-AU.
Wajumbe walimteuwa Mugabe kwa kauli moja katika mkutano wa AU unaoendelea mjini Addis Ababa-Ethiopia.
Sasa Mugabe amechukua mahala pa mwenyekiti anayeondoka wa muungano huo, Nkosazana Dlamini-Zuma.
Uteuzi wa Mugabe kuongoza muungano huo mkubwa ulio na wanachama zaidi ya arubaini, sasa umeingiza doa ndani ya AU, kwani Mugabe hana uhusiano mzuri na mataifa ya Magharibi, hasa baada ya kukaa uongozini tangu Zimbabwe ilipojipatia uhuru mnamo mwaka wa 80.
SWALI: Aliyeteuliwa kuwa mwenyekiti mpya AU ni nani?
a. Rais MUGABE
b. John Makini
c. R. Kelly
Kujibu swali hili ushinde na kuwa mfukuaji wetu bora wa wiki bofya hapa
SWALI: Aliyeteuliwa kuwa mwenyekiti mpya AU ni nani?
a. Rais MUGABE
b. John Makini
c. R. Kelly
Kujibu swali hili ushinde na kuwa mfukuaji wetu bora wa wiki bofya hapa
Daaaaaaa;Aliyekuwa kiongozi wa makaburu aachiliwa
Kiongozi wa zamani wa utawala wa kiimla wa makaburu nchini Afrika Kusini na ambaye alikuwa kinara wa kuongoza kitengo hatari cha kuwatesa watu weusi, Eugene de Kock, amesamehewa, kuhurumiwa na kuondolewa gerezani.
Eugene Alexander de KOCK alikuwa akitumikia hukumu ya mauwaji na mateso kwa wakereketwa wengi wa chama cha ANC, lakini sasa waziri wa haki na sheria Nchini Afrika Kusini, Michael Masutha, amesema kuwa de Kock ameachiwa huru kwa manufaa ya umoja wa kitaifa.
Alikuwa ametubu mbele ya tume ya haki na maridhiano kwamba alikuwa amesababisha zaidi ya vifo vya watu mia moja na pia kuhusika katika vitendo vya kuwatesa watu kinyama na ufisadi, hasa akiwalenga waliokuwa wakipinga utawala wa ubaguzi wa rangi.
Kanali huyo wa zamani wa polisi aliyekuwa na mataji mengi mno alisamehewa kwa mengi ya makosa aliyofanya, lakini akazuiliwa gerezani kwa makosa dhidi ya binadamu kabla ya kufungwa jela maisha.
18+: Dunia imekwisha, Kijana mtanashati afa aoza kwa vibibi vizee
KYLE JONES wa Pittsburgh, Pennysylvania, nchini Marekani, aliye na umri wa miaka 31, ameelezea kuvutiwa kwake na wanawake ambao wanamzidi umri kwa makumi kadhaa ya miaka. Kijana huyo ameweka wazi kwamba katika kipindi cha miaka mitano iliyopita, hajafanya mawasiliano yoyote ya kimapenzi na mwanamke aliye chini ya umri wa miaka 60.
Kyle ambaye alifichua hayo jana kipindi maalum cha kituo cha televisheni cha TLC kiitwacho ‘My Strange Addiction’ (Tamaa Yangu ya Ajabu), alisema mpenzi wake mzee zaidi wa kike ana umri wa miaka 91.
“Nawapenda wazee wa kike kwa kila kitu. Napenda harufu yao, napenda kuwa karibu nao na hisia zao,” alisema katika kipindi hicho kijana huyo ambaye alipokuwa na umri wa miaka 18 alikuwa tayari amepata mpenzi wa kike aliyekuwa na umri wa miaka 50.
Kyle alianza kuvutiwa na wanawake wazee akingali shuleni ambapo mtu wa kwanza kumvutia alikuwa ni mwalimu wake aliyekuwa na umri wa miaka 65 wakati huo.
“Nilimpenda kwa nywele zake nyeupe, umbo lake, na kila kitu,” anasema.
Subscribe to:
Posts (Atom)





.jpg)
.jpg)
.jpg)
.jpg)
.jpg)
.jpg)
.jpg)
.jpg)
.jpg)





