2014-12-31

Nishida;Lundenga alia hujuma

Dar es Salaam. Siku moja baada ya Baraza la Sanaa la Taifa (Basata), kuifungia Kampuni ya Lino International kuendesha mashindano ya Miss Tanzania kwa miaka miwili, Mkurugenzi wa kampuni hiyo, Hashim Lundenga amesema hatua hiyo imefikiwa kutokana na shinikizo kutoka kwa baadhi ya watu wenye dhamira ya kuitoa kwenye mstari wa mafanikio sanaa ya urembo nchini. 



Lundenga alisema jana uamuzi wa Basata ni utekelezaji wa dhamira ya wachache walioamua kuhakikisha Miss Tanzania inapotea kwenye ramani ya burudani nchini.


Lundenga alisema uamuzi huo wa upande mmoja, haujaangalia mafanikio ya mashindano hayo kwa miaka 21 tangu kuanza kwake na wala hatima yake baadaye.


“Niseme kweli, kwa mtu mwenye mapenzi ya kuona sanaa ya urembo inasonga mbele kwa mafanikio, kamwe hawezi kuchukua uamuzi wa kukomoa kama huu, ila kwa watu wachache walioamua kuharibu taswira ya mashindano kwa sababu zisizo na uzito, wanaweza kufanya hivyo,” alisema Lundenga.


Aliongeza: “Siko hapa kutaja majina ya watu waliojipanga kuharibu mashindano haya, lakini kwa akili isiyohitaji kazi kubwa kufikiria jambo rahisi kama hili, haiwezi kupata tabu kuamini ukweli kwamba kuna watu nyuma ya uamuzi huu wa Basata.” 



Lundenga alisema wameshangazwa na uamuzi huo wa kufungiwa, kwani umekuja katika mazingira yasiyoeleweka ambayo hayakuwapa fursa ya kujieleza.


“Tumefanya mashindano haya kwa mafanikio kwa miaka zaidi ya 20, iweje leo tunapewa adhabu kubwa kiasi hicho kwa makosa madogo,” aliongeza Lundenga.


Akifafanua, Lundenga alisema Novemba 21 mwaka huu, walipewa barua ya onyo yenye vipengele vinne na kutakiwa kuvishughulikia kwa ajili ya msimu wa mwakani, lakini Desemba 22 mwaka huu walipewa barua ya kutakiwa kusimamisha mashindano.


“Kuna tatizo hapa. Leo unapewa barua ya onyo kabla hujafanya chochote unapewa barua ya kusimamishwa tena bila hata kupewa nafasi ya kujitetea. Ni aina gani ya uamuzi kama si kuwa na watu wenye nia mbaya na mashindano haya,” alisema.

Watu Hoi;Mapinduzi yatibua ratiba ligi

Dar es Salaam. Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) limepangua ratiba ya Ligi Kuu ya Tanzania Bara ili kuziwezesha timu nne kushiriki Kombe la Mapinduzi linalotarajiwa kuanza kesho kwenye Uwanja wa Amaan, Zanzibar. 



Tanzania Bara itawakilishwa na Yanga, Simba, Azam FC na Mtibwa Sugar katika mashindano hayo ya maadhimisho ya Mapinduzi ya Zanzibar.


Mkurugenzi wa Mashindano wa TFF, Boniface Wambura alisema jana kuwa kutokana na timu hizo kushiriki katika mashindano hayo, mechi zao za raundi ya tisa na 10 ya Ligi Kuu zitachezwa baada ya timu hizo kumaliza michuano hiyo.


Wambura alisema mechi za ligi ambazo hazitachezwa wiki hii ni kati ya Azam na Mtibwa Sugar, Mbeya City na Yanga, na ile kati ya Mgambo Shooting na Simba. Mechi za wiki ijayo zinazopisha michuano hiyo ni kati ya Kagera Sugar na Azam, Coastal Union na Yanga, Mbeya City na Simba na ile ya Mtibwa Sugar na Tanzania Prisons.


Mwenyekiti wa Kamati ya Maandalizi ya Kombe la Mapinduzi, Sherry Khamis alisema timu zote zitakapokuwa visiwani na hapo ndipo ratiba kamili ya mashindano hayo itakapotolewa. 



Khamis alisema kutokana na taratibu ngumu walizopewa na timu za nje, mwaka huu mashindano hayo yatashirikisha timu moja tu kutoka nje ya mipaka ya Tanzania.


“Mabingwa watetezi tu KCCA ya Uganda ndiyo itashiriki, tulikuwa na maongezi na timu ya Ulinzi ya Kenya, hata hivyo hatukuweza kufikia mwafaka kutokana na masharti magumu,” alisema Khamis.


Alizitaja timu nyingine kuwa ni KMKM, JKU, Mafunzo, Mtende na Shaba FC. Alisema ratiba yao itakuwa na mechi mbili kwa siku yaani jioni na usiku.


Mshindi wa kwanza atazawadiwa kitita cha Sh10 milioni na wa pili Sh5 milioni, pia kutakuwa na zawadi za mfungaji bora na kipa bora.

mapema; Hakimu ajitoa kesi ya kina Sheikh Farid,

Kiongozi wa Jumuiya ya Uamsho na Mihadhara ya Kiislamu (Jumiki) visiwani Zanzibar, Sheikh Farid Ahmed
Hakimu Mkazi wa Mahakama Kisutu jijini Dar es Salaam, Hellen Riwa, amejitoa kusikiliza kesi ya ugaidi inayomkabili kiongozi wa Jumuiya ya Uamsho na Mihadhara ya Kiislamu (Jumiki) visiwani Zanzibar, Sheikh Farid Ahmed na wenzake 21.


Hakimu Riwa amechukua hatua hiyo wakati upande wa washtakiwa ukiitaka mahakama imbadilishe kwa kutokuwa na imani naye.

Oktoba 1, mwaka huu, Hakimu Riwa alitoa uamuzi juu ya maombi yaliyowasilishwa na upande wa utetezi ambayo ni pamoja na kufutwa kwa kesi hiyo kwa madai kuwa hati ya mashtaka ilikuwa haifafanui maeneo wanakodaiwa washtakiwa hao kujihusisha na ugaidi na Mkurugenzi wa Mashtaka kushindwa kueleza mashtaka yanawakabili washtakiwa hao.

Akitoa uamuzi wa kujiondoa katika kesi hiyo jana, Hakimu Riwa, alisema mahakama hiyo haina mamlaka ya kisheria ya kujibu maombi hayo ya upande wa utetezi yaliyowasilishwa Septemba 19, mwaka huu na Jaji Dk. Fauz Twaib wa Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam.


Katika ombi hilo, upande huo ulimtaka hakimu huyo kutoa uamuzi kuhusu maombi yake dhidi ya wateja wake hao.

Upande huo, ukiongozwa na Wakili, Abubakar Salim akisiadiwa na Abdallah Juma, Ubaidu Hamidu na Abdul Fatah Abdallah, uliiomba mahakama hiyo ibadilishe hakimu mwingine wa kuisikiliza kesi hiyo kwa madai kuwa Hakimu Liwa aliamuru irudishwe Mahakama Kuu.

Nalo Jopo la Mawakili wa Serikali likiongozwa na Wakili Mwandamizi Mkuu wa Serikali, Benard Kongola, Peter Njike na George Barasa, lilidai kuwa ombi hilo halina msingi kwa kuwa Mahakama Kuu iliaagiza uamuzi utolewe na Mahakama ya Kisutu lasivyo, wakiendelea kufanya hivyo watamaliza mahakimu wote.

Hakimu Riwa alisisitiza kuwa hawezi kutoa uamuzi juu ya maombi hayo ya upande wa utetezi huku akisisitiza Januari 13, mwakani kesi hiyo itatajwa mbele ya hakimu mwingine atakayepangwa kuisikiliza.

Katika shtaka la kwanza, inadaiwa kuwa washtakiwa hao kati ya Januari 2013 na Juni mwaka huu katika maeneo ya ndani ya Jamhuri ya Muungano ya Tanzania, walikula njama na kuingiza watu nchini kushiriki vitendo vya kigaidi.

Katika shtaka la pili, washtakiwa hao wanadaiwa kuwaingiza watu hao nchini kushiriki vitendo vya ugaidi huku wakijua ni kosa kisheria.

Vilevile shtaka la tatu, washtakiwa Farid na Mselem, wanadaiwa kuwa kati ya Januari 2013 na Juni 2014 katika maeneo ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, waliwaajiri Sadick Absaloum na Farah Omary kushiriki katika kutenda vitendo hivyo vya kigaidi.

Kwa upande wa shtaka la nne, mshtakiwa Farid, anadaiwa kuhifadhi watu waliotenda vitendo vya kigaidi huku akijua ni kosa kwa mujibu wa sheria.

Washtakiwa wengine katika kesi hiyo ni Jamal Swalehe, Nassoro Abdallah, Hassan Suleiman, Anthari Ahmed, Mohammed Yusuph, Abdallah Hassan, Hussein Ally, Juma Juma.

KITIM TIM;WATU WANNE WANASHIKILIWA NA JESHI LA POLISI KWA KUTOROKA NA ALBINO MKOANI MWANZA



Jeshi la Polisi mkoani Mwanza linawashikilia watu wanne akiwemo baba mzazi wa mtoto mwenye ulemavu wa ngozi Albinism aliyetekwa nyara na watu wasiojulikana usiku wakiwa wamelala na kuondoka naye kusikojulikana hali iliyozua hofu kubwa kwa jamii.
 

Amebainisha hayo kamishina msaidizi mwandamizi ambaye ni kamanda wa polisi mkoa wa Mwanza Bw.Valentino Mulowola wakati akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake amemtaja mtoto wa kike aliyetekwa nyara mwenye umri wa miaka minne Pendo Emmanuel mkazi wa kijiji cha Ndambi kata ya fukalo tarafa ya mwamashimba wilayani kwimba ambaye ni mlemavu wa ngozi amesema kuwa tarehe 27 Desemba mwaka huu majira ya saa nne na dakika 30 za usiku watu wasiojulikana walivamia nyumba ya Bw.Emmanuel Shilinde kwa kupiga jiwe mlango na kuvamia kisha wakamchukua mtoto mmoja kati ya watoto watatu waliokuwemo ndani ya nyumba hiyo kisha wakatoweka naye kusiko julikana.

Kufuatia hali hiyo makao makuu ya jeshi la polisi Tanzania imetuma timu ya askali upelelezi watakao shirikiana na askari polisi mkoa wa Mwanza kuwasaka wahalifu walio husika kumteka nyara mtoto na kutoweka naye 
pasipojulikana pamoja na kutoa ahadi ya zawadi ya fedha kiasi cha shilingi milioni tatu kwa yeyote atakaye fanikisha kukamatwa kwa wahalifu hao ambapo kikosi hicho kwa pamoja kimewatia mbaloni wahamiaji haramu saba raia wa Ethiopia na watanzania wawili wanashikiliwa kwa tuhuma za kusaidia wahamiaji haramu hao kuingia nchini kinyume cha sheria za nchi. Posted by 

JESHI LA POLISI LASHIKILIA WATU WANNE KWA KUTOROKA NA ALBINO MKOANI MWANZA




Jeshi la Polisi mkoani Mwanza linawashikilia watu wanne akiwemo baba mzazi wa mtoto mwenye ulemavu wa ngozi Albinism aliyetekwa nyara na watu wasiojulikana usiku wakiwa wamelala na kuondoka naye kusikojulikana hali iliyozua hofu kubwa kwa jamii.
 

Amebainisha hayo kamishina msaidizi mwandamizi ambaye ni kamanda wa polisi mkoa wa Mwanza Bw.Valentino Mulowola wakati akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake amemtaja mtoto wa kike aliyetekwa nyara mwenye umri wa miaka minne Pendo Emmanuel mkazi wa kijiji cha Ndambi kata ya fukalo tarafa ya mwamashimba wilayani kwimba ambaye ni mlemavu wa ngozi amesema kuwa tarehe 27 Desemba mwaka huu majira ya saa nne na dakika 30 za usiku watu wasiojulikana walivamia nyumba ya Bw.Emmanuel Shilinde kwa kupiga jiwe mlango na kuvamia kisha wakamchukua mtoto mmoja kati ya watoto watatu waliokuwemo ndani ya nyumba hiyo kisha wakatoweka naye kusiko julikana. 


Kufuatia hali hiyo makao makuu ya jeshi la polisi Tanzania imetuma timu ya askali upelelezi watakao shirikiana na askari polisi mkoa wa Mwanza kuwasaka wahalifu walio husika kumteka nyara mtoto na kutoweka naye pasipojulikana pamoja na kutoa ahadi ya zawadi ya fedha kiasi cha shilingi milioni tatu kwa yeyote atakaye fanikisha kukamatwa kwa wahalifu hao ambapo kikosi hicho kwa pamoja kimewatia mbaloni wahamiaji haramu saba raia wa Ethiopia na watanzania wawili wanashikiliwa kwa tuhuma za kusaidia wahamiaji haramu hao kuingia nchini kinyume cha sheria za nchi.

Afunguka;Rais Jammeh Bado niko mamlakani'




Rais wa Gambia Yahya Jammeh

Rais wa Gambia amesema kuwa bado analiongoza taifa hilo la Afrika magharibi baada ya vikosi vyake vya usalama kutibua jaribio la mapinduzi.


Yahya Jammeh amesema kuwa kamanda mmoja wa jeshi wa zamani alijaribu kuchukua udhibiti wa taifa hilo alipokuwa ziarani Ufaransa.

Hatahivyo hajulikani aliko.Milio mikali ya riasi ilizuka karibu na makao ya rais katika mji mkuu.

Bwana Jammeh alichukua mamlaka kupitia mapinduzi mwaka 1994 na wapinzani wake wamekuwa wakimkosoa kwa uongozi wake wa kiimla.

Duru za kidiplomasia na zile za kijeshi zinasema kuwa wanajeshi kutoka kwa jeshi la ulinzi wa rais wanadaiwa kufanya shambulizi hilo katika makao ya rais mjini Banjul mapema siku ya jummane.
 

Serikali imekana kwamba kulikuwa na jaribio la mapinduzi katika taarifa iliotangazwa katika radio ya taifa.

Hatahivyo,bwana Jammeh baadaye alikiri kuhusu shambulizi hilo na kusema kuwa wanajeshi waaminifu wa Lamin Sanneh aliyemtaja kama mwenye aibu walivamia mji mkuu wa Gambia kutoka Senegal katika jaribio la kutaka kuipindua serikali yake.

Amesema kuwa wavamizi hao hatahivyo walikabiliwa na vikosi vya usalama na kuwaua wanne kati yao huku wengine wanne zaidi wakikamatwa.

DUU;.Ndoa za jinsia moja zafanyika Uskochi





Joe na mwenzake Brown wakifunga ndoa nchini Uskochi

Harusi ya kwanza ya watu wa jinsia moja imefanyika huko Uskochi .

Joe Schofield na Malcom Brown walifunga ndoa katika sherehe iliofanyika katika eneo la Trade Hall Glasgow huku Susan na Gerrie Douglas -Scott wakifanya harusi yao katika eneo la faragha mjini humo.


Sheria hiyo mpya ya watu wa jinsia moja ilianza kufanya kazi Uskochi mapema mwezi huu.

Sherehe hizo zilihudhuriwa na waziri wa kwanza wa Uskochi. Susn na mwenzake Gerrie wakifanya ndoa yao huko Uskochi 
Nicola Sturgeon na mashirikishi wa chama cha Green Party Patrick Harvie MSP walishuhudia ndoa ya Susan na Gerrie naye mshairi wa kitaifa wa Uskochi Liz Lochhead na waziri wa serikali ya Uskochi Marco Biagi MSP wakihudhuria sherehe ya bwana Schofield na mwenzake bwana Brown.

Susan mwenye umi wa miaka 54 na Gerrie Douglas-Scott mwenye umri wa miaka 59 wanaishi mjini Galsgow ambapo walikutana miaka 18 na wana watoto wakubwa watano.

Walioana mwaka 2006 na kuamua kufanya sherehe mwaka huu.

Kume Kucha;Makundi ya urais CCM yaitafuna jumuiya ya wanafunzi wa vyuo

0





Dar es Salaam. Mbio za urais 2015 zinaendelea kushika kasi. Wanasiasa wanapigana vikumbo kutafuta kuungwa mkono na vyama vyao kwa nia ya kuendelea kushika dola kwa wale waliopo madarakani na waliopo nje wakijaribu kujiimarisha kwa kujiongezea wafuasi ili waweze kupata ridhaa ya kuongoza.


Vita vya wazi ni baina ya chama tawala cha CCM na kambi ya upinzani kupitia ushirikiano wao walioupa jina la Ukawa.


Kwa ujumla wanasiasa kutoka makundi haya wameelekeza nguvu zao katika kusaka uungwaji mkono kwa vijana kwa kile wanachoeleza kuwa ndilo kundi pekee lenye uwezo wa kushawishi idadi kubwa ya watu wa kada zote kwa lengo la kujizolea ushindi katika chaguzi zijazo. 



Eneo pekee lenye vijana wa kada na hulka tofauti ni ndani ya jumuiya za wanafunzi nchini. Na kutokana na ukweli huo, tayari CCM imepiga hodi ndani ya Jumuiya ya Wanafunzi wa Taasisi za Elimu ya Juu nchini (Tahliso), kutafuta kuungwa mkono.


Hatua ya CCM kujipenyeza katika jumuiya hiyo ya wanafunzi, imesababisha mpasuko mkubwa uliopo kwa viongozi na wajumbe wa Tahliso na wanafunzi kwa ujumla wake. 



Katika kudhihirisha hilo, uongozi wa Tahliso chini ya uenyekiti wa Musa Mdede imemuondoa madarakani makamu mwenyekiti, katibu mkuu, naibu katibu na mwenyekiti wa Baraza Kuu la Tahliso (seneti) kwa madai ya kukiuka maadili ya uongozi.


Mwananchi ilifanya mahojiano maalumu na Mdede kutaka kujua nini sababu za hali iliyosababisha kufanya mabadiliko ya uongozi wa juu wa jumuiya hiyo ya wanafunzi.


Swali: Kuna ukweli gani kuhusu madai kuwa baadhi ya viongozi Tahliso wamevuliwa madaraka?


Jibu: Ni kweli. Wapo baadhi ya viongozi wa jumuiya hii ambao tumewavua uongozi. Sababu ya kufanya hivyo ni kuwa walikosa uvumilivu na hawakutambua majukumu yao ndani ya Tahliso.


Tumebaini siyo mara moja kuwa miongoni mwa viongozi wanafunzi waliotekwa na makundi yanayompigia kampeni za urais mmoja kati ya vigogo wa CCM yumo ndani ya Tahliso. Tulishasema kampeni hizo wafanye nje na siyo kuzileta kwa wanachama wa Tahliso.


Julai 31, mwaka huu tuliwakuta wakishiriki mkutano na kigogo huyo katika Hoteli ya Valley View hapa jijini Dar es Salaam. Kundi jingine likawachukua wenyeviti 10 wa vyuo mbalimbali na kushawishiwa watangaze mbele ya vyombo vya habari kwamba jumuiya ya Tahliso haina uongozi.


Baadhi yao, wakapewa tisheti zenye ujumbe wa kumpigia kampeni kigogo huyo, hali ambayo ilikuwa kinyume na Sheria ya Vyuo Vikuu ya 2005 pamoja na Katiba ya Tahliso.

Kweli Kabisa;Ufisadi ni mbolea ya kuchochea ugaidi






Huko Nigeria mwanajeshi hunyongwa anapokataa kupigana dhidi ya kundi la kigaidi la Boko Haram. Na karibuni huko Kenya ilipitishwa Sheria ya Usalama, ambayo pindi busara haitatumika itaweza ikaipeleka nchi hiyo pabaya na hata kuonekana mbele ya watu wa ndani na nje kwamba ni dola ya kipolisi.


Serikali za nchi hizo mbili za Kiafrika- moja iko Afrika Magharibi na nyingine Afrika Mashariki, zina kila sababu ya kupambana na kuwazuia magaidi wanaohatarisha usalama wa raia na mali zao. Lakini mara kadhaa malengo mazuri humalizikia kwa matokeo mabaya na vurugu, ikiwa uangalifu hauchukuliwi. 



Pia ikiwa watekelezaji wanakuwa wakakamavu na kutokuwa tayari kuzidurusu hatua zao kila wakati kama zinaambatana na tunu muhimu za kuheshimu utu wa mwanadamu. Kuna wasiwasi kwamba hatua zilizochukuliwa na serikali za nchi hizo mbili zinakosa malengo na hazitasaidia kuondoa mzizi wa fitina wa ugaidi.


Mashambulzi ya kigaidi


Katika kisa cha karibuni cha mashambulio ya magaidi huko Nigeria ambayo yametia fora mwaka 2014, magaidi wa Boko Haram waliwateka nyara watu kadhaa. Msemaji wa Serikali ya Nigeria alikuwa hana zaidi la kusema ila kushtushwa, kusikitishwa na kukilaumu kitendo hicho.


Baada ya shambulio hilo lililofanywa karibu na Gumsuri, kijiji kilichoko katika Mkoa wa Kaskazini mwa Borno, mambo yalibadilika na kuwa vurugu tupu. Barabara nyingi zilikuwa hazipitiki na mawasiliano kupitia simu za mikononi yalikuwa hayawezekani. Kwa hakika ilichukua siku kadhaa hadi sura kamili ya tukio hilo kupatikana katika mji mkuu wa Abuja.


Inasemakana wanavijiji walikusanywa na kuhamishwa kama ng’ombe, si chini ya 35 kati yao waliuawa kwa risasi. Habari nyingine zinasema wanawake na wasichana 200 walipakiwa katika malori na haijulikani walikopelekwa.


Japokuwa kikundi cha Boko Haram halijakiri kuhusika, lakini mabingwa wa harakati za magaidi wanasema shambulio hilo jipya lina sura kwamba Boko Haram ndio walioufanya ukatili huo. Idadi ya ukatili unaofanywa na kikundi hicho, ambacho bila ya haki kinajigamba kinausemea Uislamu, imeongezeka hivi karibuni.


Mwaka wa 2014 maelfu ya watu wasiokuwa na hatia wameuawa Nigeria na kundi hilo, ambalo tangu mwaka 2009 limekuwa likidai kuweko dola huru la Ukhalifa ( Mrithi wa Mtume Muhammad). Kwa mujibu wa jumuiya zinazotoa misaada, Wanigeria milioni 1.5 wamekimbilia kwenye mikoa ilio na amani au wameelekea nchi jirani kutokana na kitisho cha Boko Haram.


Jeshi la Nigeria linaonekana kuelemewa, haliwezi kuwalinda raia na zaidi haliungwi mkono na raia. Linakosa silaha za kisasa. Maafisa pamoja na wanajeshi wao kwa muda mrefu wamekuwa wakilalamika kwamba hawana silaha za kutosha kuweza kukabiliana na kuwashinda wapiganaji wa Boko Haram walio na silaha za kutosha.


Nyingi ya silaha waliozonazo Boko Haram ni zile zilizoachwa na wanajeshi wa serikali wanaokimbia kutoka uwanja wa mapigano. Mara kadhaa kumetokea visa vya wanajeshi wa serikali huko Borno kukataa kutii amri za wakuu wao. Wanajeshi hao husimamishwa mbele ya mahakama za kijeshi wakishtakiwa kuwa waoga mbele ya adui au kufanya uasi na 54 kati yao wameshapewa hukumu ya kifo.


Lakini haifikiriwi kwamba hukumu kali za kifo dhidi ya wanajeshi waoga itaibadilisha hali ya mambo inayozidi kuwa mbaya huko Nigeria. Ingekuwa bora kuushughulikia mzizi wa tatizo hilo la ugaidi wa Nigeria.

POLENI;Kenya na ubovu wa upinzani, Katiba na tatizo la usalama

Tangu wiki iliyopita, Bunge la Kenya limeendelea kujadili muswada wa mabadiliko ya Sheria (Security Laws Amendment Bill 2014) ambao ulitarajiwa kuleta mabadiliko makubwa katika mustakabali mzima wa usalama wa nchi. 



Ikumbukwe Kenya imekuwa ikikabiliana na mfululizo wa mashambulizi kutoka kikundi cha kigaidi cha Al Shabaab kwa zaidi ya miaka miwili sasa. Zaidi ya watu 200 wanakisiwa kuuawa kinyama hadi sasa.


Muswada huu uliishia kwa wabunge kutwangana ngumi bungeni, jambo ambalo ni la aibu mbele ya Wakenya.


Muswada huo ulilenga vyombo vyote vya usalama, jeshi, polisi, uhamiaji na Huduma ya Intelijensia ya Taifa (National Intelligence Services), kuwa na mamlaka ya kukabiliana na ugaidi.


Sheria hii ni kali dhidi ya watumishi wa serikali wanaotoa vitambulisho na nyaraka muhimu, wananchi wanaowahifadhi na kuwasaidia magaidi na taasisi za kidini na kiraia zinazochochea vitendo vya kigaidi.


Kabla ya kupitishwa muswada huo, vitengo hivyo vilikuwa na uwezo mkubwa wa kukabiliana na magaidi lakini baada ya kuvurugwa na katiba mpya, mfumo mzima wa usalama unaonekana kuyumba.


Mabadiliko mengine ni kama vile kifungo cha miaka isiyozidi mitatu kwa kosa la kutoa habari inayoweza kukwamisha jitihada za kukabiliana na ugaidi.


Vilevile, kuna kifungo cha miaka isiyozidi 20 kwa matumizi ya bomu katika mashambulizi ya kigaidi.


Mtu yeyote atakayepatikana na silaha ndani ya nyumba za ibada au kuhubiri falsafa za kigaidi au uchochezi wa kidini atatumikia kifungo cha miaka isiyozidi 30. 



Pia, muswada huo ulikusudia kumpa Rais Kenyatta mamlaka ya kuteua mkuu wa Jeshi la Polisi (IGP) baada ya mamlaka kuondolewa na katiba mpya na kuipa tume mamlaka hiyo.


Tatizo la usalama Kenya linatokana na katiba ambayo iliweka sheria ambazo zinaifunga mikono Serikali kuwafuata na kuwahukumu magaidi au watu wenye nia mbaya na kuathiri mtiririko mzima wa usalama. 



Kwa mfano, katiba inasema mtu yeyote asizuiliwe na polisi zaidi ya saa 24, lakini muswada unapendekeza kushikilia mtuhumiwa wa ugaidi zaidi ya muda huo.

HURUMA;KUNDI LA ISIS LAWACHINJA WAPIGANAJI WAKE ZAIDI YA 120 KWA KUJARIBU KUTOROKA



Wapiganaji wa ISIS wakiua kundi la watu kwa risasi©RT
Kundi hatari linalodai kutetea na kufuata haki za dini ya kiislamu linalopigana nchini Iraq na Syria la Islamic State limewanyonga wapiganaji wake wa kigeni zaidi ya120 kufuatia wapiganaji hao kutaka kuondoka na kurudi makwao na kuachana na kundi hilo. 

Wapiganaji waliouwawa ni waliokuwa wakitumikia kundi hilo katika mji wa Raqqa nchini Syria walikamatwa wakijaribu kutoroka kurudi makwao kama chanzo cha taarifa hii kilipozungumza na mwandishi wa  ambaye amedai watu wanaopinga vitendo vya ISIS na utawala wa Rais Bashar al-Assad amesema watu waliouwawa walikuwa wakijaribu kutoroka baada ya ISIS kutoa mwongozo mpya wa wapiganaji wake katika kuwazuia kukimbia. 
 

Ingawa kuna wapiganaji wengi kutoka sehemu mbalimbali duniani wanaojiunga na kundi hilo kwakuhadaiwa kwamba ISIS itawasaidia kuielewa vyema dini ya kiislamu na mara baada ya kujiunga wanajikuta walidanganywa na matokeo yake wanajiingiza katika vitendo vya kikatili vya mauaji vinavyofanywa na wapiganaji wa kundi hilo na kutaka kujiondoka kitu ambacho hakiwezekani. Aidha taarifa hiyo inasema wapiganaji mara wanapojiunga hutakiwa kupigana na kutojitoa katika kundi hilo la linalodai kufuata misingi ya dini na kupokea vitisho kutoka kwa wapiganaji wengine wa ISIS kwamba watauwawa endapo watajaribu kutoroka. 

Kumekuwa na kundi kubwa la vijana na watu wa makamo sehemu mbalimbali duniani ambao huadaiwa na kundi hilo la ISIS likiwashawishi kwa njia ya mtandao au kupitia wawakilishi wao waliopo nchi mbalimbali kwa kificho ili kwenda kujiunga nao katika mapigano ili kuendeleza ama kudumisha dini ya Kiislamu na matokeo yake hujikuta wamehadaiwa na kujiingiza kwenye mauaji yasiyo na hatia ya kuua hata watoto kwakisingizio cha dini, kitendo ambacho kimekuwa kikipingwa na waumini mbalimbali wa dini ya kiislamu na dini nyingine duniani.


Baada ya kuanguka CCM-Wassira ataja sababu kashfa ya Escrow

 
Mh. Stephen Wassira, amekiri kuwa kutochukua hatua za mapema kuhusu sakata la uchotwaji wa fedha katika akaunti ya Tegeta Escrow ni moja ya sababu ambayo imesababisha chama hicho kutofanya vizuri katika uchaguzi wa serikali za mitaa.

Mh,Wassira ambaye pia ni Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Mahusiano na Uratibu ameyasema hayo nyumbani kwa Baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere Kijijini Butiama, ambapo amesema kitendo cha serikali kushindwa kutoa taarifa kwa wakati kimechangia kuwachanganya Watanzania kuhusu sakata hilo.
 

Hata hivyo mjumbe huyo amesema hivi sasa taifa linakabiliwa na wimbi kubwa la baadhi ya viongozi wake kukosa uzalendo na uadilifu huku wakitanguliza mbele maslahi binafsi kitendo ambacho amesema kinaondoa dhana nzima ya kumuenzi baba wa taifa
 

Naye mmoja ya watoto wa baba wa Taifa Mh. Makongoro Nyerere, ametumia mazungumza hayo na Mh. Wassira kuitahadharisha CCM, kuwa endapo itashindwa kudhibiti vitendo vya rushwa, matumizi mabaya ya fedha katika uchaguzi kuna hatari ya kuwagawa watanzania na kufanya CCM kupoteza dola katika uchaguzi mkuu ujao.

Ni shiiiiiiiiiiiida!!!!!!! Baada ya Kumzawadia wema Sepetu Gari ya Bei Kubwa iliyoleta Utata Martin Kadinda anunua gari mpyaaa!

Baada ya Martin Kadinda Kumzawadia Gari ya Gharama Wema Sepetu siku ya Sherehe ya kuzaliwa kwake iliyoleta utata naye ameamua kununua gari kali aina ya Primera Kuwakata Watu Midomo walio shangaa kwa yeye Kumpa mtu zawadi ya gari ya gharama wakati yeye hana ... 



Jionee Picha hapo chini na Ujumbe aliondika kwenda kwa mashabiki wake:

                           

Ni perampera!!!!!!!!!!!!!!!!! Polisi Yatangaza Msako kwa Wanawake Wanaofanya Biashara ya Ngono


 
Polisi mkoani Tanga wamesema wataendesha msako wa kuwakamata watu wanaofanya biashara ya ngono katika nyumba za starehe na mitaa maarufu kwa biashara hiyo.

Msako huo unatokana na malalamiko ya muda mrefu ya wakazi wa Jiji la Tanga hususan wanaoishi mitaa ya Centrol na Ngamiani ambako biashara hiyo inadaiwa kukithiri.

Akizungumza na Mwandishi hivi karibuni, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Tanga, Freisser Kashai alisema wamepokea malalamiko hayo muda mrefu, walishindwa kuchukua hatua mara moja kwa kuwa walikuwa wakiyafanyia uchunguzi.


Alisema baada ya kumalizika kwa uchunguzi wao, wamejipanga kuwakamata wote wanaohusika ili hatua za kisheria zichukuliwe dhidi yao. Kamanda huyo alisema kuendelea kuiacha ishamiri inachangia kuporomosha maadili ndani ya jamii.

Kamanda Kashai alisema cha kusikitisha, biashara hiyo sasa inafanywa mpaka na watoto wadogo wenye umri wa kwenda shule na wanafunzi wanaosoma shule za bweni ambao wengi hutoroka nyakati za usiku na kwenda kujiuza kwenye nyumba za starehe.

Alisema polisi wana taarifa zote za majengo na maeneo kunakofanyika biashara hiyo. “Operesheni yetu itaanza muda wowote kuanzia sasa, tutawakamata na kuwafikisha mahakamani,” alisema.


Akizungumzia usalama wa raia na mali zao katika sikukuu ya Mwaka Mpya, Kamanda Kashai ametoa wito kwa wakazi wa mkoa huo kutoa taarifa kwa polisi pale watakapobaini viashiria vya uhalifu katika maeneo yao.

“Kila mara tumekuwa na utaratibu wa kufanya mikutano na wananchi mitaani kuwaelimisha namna ya kushirikiana na Polisi kuwafichua wahalifu, hii imesaidia kupunguza matukio hayo kwa asilimia kubwa,” alisema Kashai.

HALI MBAYA YA HEWA YAKWAMISHA ZOEZI LA UOKOAJI MIILI KUTOKA AIRASIA QZ8501



Baadhi ya mabaki ya Ndege ya AirAsia yakiwa Uwanja wa Ndege wa Pangkalan Bun, Indonesia leo. 
 


Mwili wa mmoja wa watu waliokuwa kwenye ndege ya AirAsia ukielea katika Bahari ya Java.

Maofisa wa Kikosi cha Uokoaji wakiichunguza ramani inayoonyesha eneo ilipokutwa miili ya watu waliokuwa katika AirAsia.

Ndugu na jamaa wa watu waliokuwa kwenye Ndege ya AirAsia wakiwa na simanzi baada ya kupata taarifa za kupatikana kwa miili baharini. 


JITIHADA za kuopoa miili kutoka katika Ndege ya AirAsia QZ8501 iliyoanguka baharini Jumapili iliyopita ikiwa na watu 162 zimeendelea kukwamishwa na hali mbaya ya hewa.

Ndege hiyo ilianguka katika Bahari ya Java nchini Indonesia na hali ya dhoruba katika eneo la uokoaji imezidi kukwamisha zoezi hilo.

Mamlaka nchini Indonesia yamethibisha kuwa mabaki yaliyoonekana majini eneo la Borneo ni ya ndege iliyopotea ya AirAsia.

Rais wa Indonesia, Joko Widodo, ameahidi kuendelea kufanya uchunguzi wa kina kwa kutumia meli na helkopta kuhakikisha miili ya watu waliokuwa kwenye ndege hiyo inapatikana.

Maombolezo ya pamoja yanatarajiwa kufanyika leo huko Surabaya nchini Indonesia na Gavana wa Jimbo la Java Mashariki, Soekarwo ameeleza kuwa sherehe zote za Mwaka Mpya zimesitishwa kutokana na ajali hiyo ya AirAsia.

MAMBO HAYOOOOOO!!!!!!!!!!!! MATUKIO YALIYOTIKISA NCHI MWAKA 2014

Msanii wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond’ akiwa na mshindi wa shindano la Big Brothers Idris.
MWAKA 2014 unafikia tamati leo. Kwa Watanzania, kuna matukio mbalimbali yaliyojitokeza ambayo yameacha kumbukumbu kubwa kwao. Hata hivyo, yafuatayo ndiyo mambo yaliyotia fora zaidi. 


Viungo vingi vya binadamu vikiwa vimetupwa katika machimbo ya kokoto yaliyopo Bunju, Dar.

VIUNGO VYA BINADAMU VYASHTUA 

Jumatatu ya Julai 21, 2014, nchi ilipatwa na mshtuko mkubwa baada ya kusambaa kwa habari kuwa viungo vingi vya binadamu vilikutwa vikiwa vimetupwa katika machimbo ya kokoto yaliyopo Bunju, Kinondoni jijini Dar es Salaam.

Watu wengi waliamini viungo hivyo vimetokana na mauaji ya halaiki, hasa baada ya kukutwa kwa mabaki ya mikono, miguu, mafuvu, viganja na vingine vingi. Lakini baadaye ikaja kuthibitika kuwa viungo hivyo vilitupwa kimakosa na Chuo Kikuu cha Kimataifa cha Tiba na Teknolojia (IMTU), ambacho pia kinaendesha hospitali.

Viungo hivyo mbalimbali vya binadamu vilikuwa vikitumiwa kimasomo na madaktari wanafunzi, ambavyo vilipaswa kuteketezwa baada ya matumizi. Kitendo hicho kilisababisha serikali kukisimamisha kwa muda chuo hicho kutokana na uzembe huo. Viungo hivyo vya binadamu, hupatikana katika maiti mbalimbali zinazokosa ndugu wa kuwazika na hutolewa na hospitali ya Taifa Muhimbili. 


Kundi lililoitwa Umoja wa Katiba ya Wananchi (UKAWA),wakiongozwa na Mwenyekiti wa CUF, Profesa Ibrahim Lipumba.
KUZALIWA KWA UKAWA

Baada ya Rais Jakaya Kikwete kuridhia zoezi la uandikwaji wa Katiba Mpya, Tume ya kukusanya maoni chini ya uenyekiti wa Jaji Joseph Warioba ilifanya kazi yake vizuri na mwaka huu katiba hiyo ilipelekwa Bungeni ambako Bunge Maalum la Katiba lilikutana ili kupitia vifungu vyake kabla ya kuipeleka kwa wananchi kwa ajili ya kuipigia kura ya kuikubali au kuikataa.

Kulitokea malumbano makali kati ya wajumbe wa Bunge hilo juu ya vipengele kadhaa, hasa muundo wa serikali ya Jamhuri ya Muungano. Wajumbe waliotokana na Chama Cha Mapinduzi, walipendezwa na muundo wa serikali mbili kama ilivyo hivi sasa, wakati wapinzani walitaka serikali tatu.

Misimamo hiyo ilileta utengano mkali kiasi kwamba wajumbe wa upinzani wakiongozwa na Mwenyekiti wa CUF, Profesa Ibrahim Lipumba kuamua kususia vikao hivyo, wakipinga kile walichokiita uchakachuaji wa rasimu ya katiba ya Jaji Warioba. Ususiaji huo ulisababisha kuanzishwa kwa kundi lililoitwa Umoja wa Katiba ya Wananchi (UKAWA).

                                Jaji Warioba

Kuanzishwa kwa umoja huo uliovihusisha vyama vya Chadema, CUF, NCCR-Mageuzi na NLD, kulisababisha kundi hilo kukubaliana kusimamisha mgombea mmoja katika chaguzi zijazo, wakianzia na uchaguzi wa serikali za mitaa uliofanyika katikati ya mwezi huu. 


JAJI WARIOBA APIGWA

Baada ya wajumbe wa Bunge Maalum la Katiba kumaliza kazi yake na kuikabidhi katiba pendekezwa kwa Rais Jakaya Kikwete tayari kwa ajili ya kuipeleka kwa wananchi ili kupigiwa kura ya maoni, kulikuwa na mkanganyiko miongoni mwa watu juu ya kilichomo ndani ya katiba hiyo, baadhi wakipinga kuondolewa kwa vifungu vingi vilivyokuwa na masilahi kwa nchi.

Miongoni mwa wanaoongoza harakati za kupinga kuondolewa kwa baadhi ya vifungu vilivyowasilishwa na Tume hiyo, ni Taasisi ya Mwalimu Julius Nyerere ambayo mara kadhaa imeandaa mijadala ya wazi, lakini wakimtumia Jaji Warioba kama msemaji wake mkuu.

Kitendo hicho kimesababisha Warioba kuonekana kama yupo katika mgogoro na chama chake na siku aliyofanyiwa fujo na kupigwa katika ukumbi wa mikutano wa Ubungo Plaza, wanaodaiwa kuwa makada wa CCM wanatajwa kuhusika. 


Aliyekuwa mshindi wa miss Tanzania 2014, Sitti Mtemvu kabla ya kuvuliwa taji.

Kitendo hicho pia kilikosolewa na wachambuzi wa habari za kisiasa wakidai ulikuwa ni udhalilishwaji wa mtu aliyewahi kuwa Makamu wa Rais na Waziri Mkuu wa Tanzania na hivyo kuhoji ulinzi wake.MISS

TANZANIA YAFUNGIWA MIAKA 2

Shindano la Miss Tanzania limejijengea heshima kwa muda mrefu tokea lilipoanza tena mwaka 1994. Ingawa kumekuwa na malalamiko ya chinichini juu ya kuwepo kwa hila, safari hii lilijikuta likipata aibu kubwa, baada ya mshindi wake wa mwaka huu, Sitti Mtemvu kudaiwa kudanganya umri hivyo kuibua sauti zilizotaka kunyang’anywa kwa taji hilo.

Baada ya skendo hiyo kuchachamaa, Baraza la Sanaa la Taifa liliendelea na uchunguzi wake dhidi ya malalamiko mengi yaliyowahi kuripotiwa na katika tukio ambalo halikutarajiwa, shindano hilo limesimamishwa kwa miaka miwili kutofanyika na sababu nyingine iliyosababisha hatua hiyo, ni kugundulika kuwepo kwa rushwa ya ngono katika hatua mbalimbali za shindano hilo linaloanzia vitongojini. 


Aliyekuwa msanii mkongwe katika uchekeshaji maehemu Said Ng’amba ‘Mzee Small’.

VIFO VYA WASANII WA MUVI NA MUZIKI

NI mwaka mwingine ambao wasanii wengi, wakiwemo wacheza filamu na wanamuziki walifariki dunia. Mei 27 mwaka huu, msanii wa Bongo Muvi, Rachel Haule alifariki katika hospitali ya Taifa ya Muhimbili. Alikwenda hospitalini kwa ajili ya kujifungua, lakini baada ya kitendo hicho hali yake ilibadilika ghafla ambapo alihamishiwa ICU na hali yake ilizidi kuwa mbaya kabla ya kupoteza maisha.

Recho alifariki wiki moja baada ya muigizaji mwingine maarufu, Adam Kuambiana kufariki ghafla. Baada ya hapo, msururu wa wasanii ulifuata akiwemo prodyuza George Tyson, msanii mkongwe katika uchekeshaji Said Ng’amba ‘Mzee Small’, mwanamuziki wa Twanga Pepeta, Khamis Kayumbu ‘Amigolas’, Side Mnyamwezi, Yesaya Ambilikile ‘YP’ , Maalim Gurumo, Amina Ngaluma, Aisha Madinda na Shem Kalenga.

6. TEGETA ESCROW NA BILIONI 306

DAVID Kafulila, mbunge wa Kigoma Kusini (NCCR-Mageuzi) alianza kama utani, akiwatuhumu vigogo wa serikali kuhusika na wizi wa shilingi bilioni 306, mali ya umma katika akaunti ya Tegeta Escrow.
 Mwanasheria Mkuu wa serikali wakati huo, Jaji Fredrick Werema akamdhihaki kwa kumuita Tumbili kabla ya kumtishia kumkata kichwa.
 Dhihaka zikaendelea kwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini, Eliakim Maswi, kuziita nyaraka alizokuwa nazo Kafulila kuwa ni makaratasi ya kufungia vitumbua.

Mbunge wa Kigoma Kusini (NCCR-Mageuzi), David Kafulila.
Kadiri muda ulivyokuwa unakwenda, ikaja kuthibitika kuwa ni kweli kulikuwa na uchotwaji wa fedha hizo isivyo halali, kitu kilichosababisha nchi kuingia katika kashfa nyingine ya mabilioni ya fedha, ukiacha EPA, Richmond, Rada na Ndege ya Rais.

Mshindo wa skendo hiyo umeondoka na vigogo watatu, waliotanguliwa na Jaji Fredrick Werema aliyejiuzulu, Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Profesa Anna Tibaijuka aliyeondolewa na Katibu Mkuu Maswi, aliyesimamishwa ili kupisha uchunguzi dhidi yake. 


HOMA YA DENGUE

Ni ugonjwa mpya ambao uliingia na kumshtua kila Mtanzania, kufuatia kasi yake ya kuua na utata wa tiba yake. Uliwafanya watu kuogopa na kuitaka serikali kuhakikisha tiba yake inapatikana mara moja ili kuondoa hofu miongoni mwa wananchi.


8. UCHAGUZI SERIKALI ZA MITAA 

INGAWA umekuwa ukifanyika kila baada ya miaka mitano, lakini uchaguzi wa serikali za mitaa mwaka huu ulipata hamasa kubwa na kufuatiliwa kwa karibu na watu wengi. Ingawa kama ilivyotegemewa, Chama Cha Mapinduzi kuibuka na ushindi, lakini hata hivyo, matokeo yake yalionyesha dalili za kuimarika kwa vyama vya upinzani baada ya kushinda viti takribani 3000 vya uenyekiti wa serikali za mitaa.

Diamond platnumz’.

Uchaguzi huo ambao ulisimamiwa na Tawala za Mikoa (TAMISEMI) iliyo chini ya ofisi ya Waziri Mkuu, ulikuwa na dosari kadhaa zilizomlazimisha Waziri wake, Hawa Ghasia, kuwasimamisha kazi Wakurugenzi, kuwafukuza na wengine kupewa onyo, kufuatia uzembe wao katika kusimamia zoezi hilo muhimu nchini.

DIAMOND, IDRIS WANG’ARA

Msanii wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond’ mwaka 2014 aliwaongoza wenzake kuing’arisha Tanzania kimataifa baada ya kufanikiwa kutwaa tuzo tano barani Afrika. Hizo ni pamoja na tatu kutoka kituo cha televisheni cha Channel O, jijini Johannesburg na The Future Awards Africa iliyofanyika Lagos, Nigeria.

Ushindi wake huo ulimfanya kupata mapokezi makubwa ya aina yake alipowasili Uwanja wa ndege wa kimataifa wa Julius Nyerere na mashabiki walimsindikiza hadi ukumbi wa Escape One kwa mi guu, umbali wa zaidi ya km 20.

Aidha kijana Idris Sultani alikuwa Mtanzania wa pili kushinda shindano la Big Brother, baada ya Richard Bezuidenhout kuibuka kinara mwaka 2011. Idris, aliyeshinda Big Brother Hotshots alijinyakulia kitita cha dola 300,000 baada ya kumbwaga Tayo Faniran wa Nigeria.

ROHO JUU;KATIBA MPYA Kura tatu zawaweka njiapanda Wazanzibari





Wananchi wa Zanzibar wapo katika matayarisho ya kupiga kura ya maoni ya Katiba Inayopendekezwa baada ya Bunge la Katiba kukamilisha majukumu yake Oktoba mwaka huu na kubakia kura ya maoni mwakani.


Upingaji wa kura utatanguliwa na elimu ya uraia ambayo itatolewa na kamati maalumu ambazo zitaundwa kwa ajili ya kufanikisha kazi hiyo mbali na makundi ya wanaharakani na vyama vya siasa. 



Kama Katiba hiyo itafanikiwa kupita, Tanzania itakuwa imeandika historia mpya baada ya miaka 50 kuandika Katiba inayotokana na ushirikishwaji wa wananchi wa pande mbili za Muungano wa Tanganyika na Zanzibar.


Maneno mawili yametawala sana katika mijadala Zanzibar hasa katika mabaraza ya kahawa na masikani watu kwa makundi ya vijana, wazee na wanasiasa wakitumia muda mwingi kubishana kama Katiba Inayopendekezwa itapita au.


Matokeo ya kura ya maoni yanasubiriwa kwa hamu kwa sababu ndiyo dira ya kutoa mwelekeo wa Uchaguzi Mkuu unaotarajiwa kufanyika Oktoba mwakani.


Makundi yaibuka


Tayari kumeibuka makundi matatu Zanzibar, kila moja likiwa na mtazamo wake kuhusu kura ya maoni.


Wapo wanaofanya kampeni ya kutaka kuungwa mkono kwa maana ya kupigiwa kura ya ndio, wengine wanaendesha kampeni ya kutaka wananchi wapige kura ya hapana, lakini kundi la tatu linalofanya kampeni ya kuwataka wananchi kususia zoezi zima la kura ya maoni itakayofanyika mwakani.

Ni noumaaaaaaaaaa!!!!!! Jay Z Ndie Aliyemtoa Bikra Beyonce Mpwa wake Avujisha Siri.



Taarifa za staa Jay Z ambazo zinasambazwa na Mpwa wake kuwa alitelekeza familia yako baada ya kuwa na mahusiano na Beyonce.
 Kwenye tweets ambayo hiyo akaunti imefungwa sasa, Ndugu huyo wa Jay Z alikaririwa kwenye moja ya tweets zake akisema akimlaumu ndugu yake kuwa alidata kwa kuwa ndiye alimvunja bikra Beyonce hii ni moja kati ya tweets zake

You changed man. Your life ain't the same since that bitch came in. Now you think your family is Tina, Solo, Julez. We aren't let in your home. 


You won't fogive Aunt Mickey, but you forgave your bitch's drunk sister. After she hit you like a bitch - man for the world to see.

Because she doesn't want you around your family and you say "yes" like you're some puppet. You spend your birthday in Iceland so we wouldn't get invited.

Shit Mama Gloria doesn't find it weird. She likes that bitch [Beyonce]. She tells TT and crew not to be immorial in school. She says 'be like Beyonce.
 
 She lost her innocence to your uncle'. Wait until your 21. Maybe that's why you're still in?I de-virgined over 4 chicks. No strings attached.

JB AAMUA KUJISAHAURISHA



Muigizaji mkongwe kwenye filamu nchini, Jacob Steven ‘JB’.
MUIGIZAJI mkongwe kwenye filamu nchini, Jacob Steven ‘JB’ ameamua kujipoteza kwa makusudi katika uigizaji akiwa na lengo la kuweka mbele kazi zinazofanywa na kampuni yake ya uzalishaji sinema ya Jerusalemu.

Akipiga stori na gazeti hili, JB alisema mwaka 2014 filamu zake tatu za Bado Natafuta, Wageni Wangu na Chausiku zilifanya vizuri sokoni. 


“Kwa asilimia 80 mwaka huu kwangu umekuwa mzuri kikazi, nimefanya kazi nzuri bila mimi kuonekana kwa sababu nataka Jerusalemu ianze halafu mimi baadaye ndiyo sababu kubwa iliyofanikisha muvi zangu zote kufanya vizuri, sitaki kuwa naonekana mara kwa mara kwenye filamu,” alisema.



GPL

WALENGWA WA MPANGO WA KUNUSURU KAYA MASKINI UNAOTEKELEZWA NA TASAF WACHIMBA MTARO WA MAJI

 Maelfu ya wakazi wa shehia ya Mpapa wilaya ya Kusini Unguja wanatarajiwa kunufaika na huduma ya maji safi na salama baada ya kukamilika kwa mradi wa maji unaotekelezwa na walengwa wa Mpango wa kunusuru kaya maskini unaoratibiwa na Mfuko wa Maendeleo ya Jamii TASAF kwa utaratibu wa ajira ya muda PWP.

Wakizungumza katika eneo la mradi baadhi ya walengwa hao wameonyesha utayari wao katika kuchimba mtaro huo huku wakiipongeza serikali kupitia TASAF kwa kubuni utaratibu huo ambao wamesema licha ya kuwaongezea fedha lakini pia utapunguza kero ya upatikanaji wa maji katika eneo lao .

Chini ya utaratibu wa ajira za muda ,walengwa kutoka kaya maskini huibua miradi katika eneo lao na kuitekeleza na kisha kulipwa ujira ikiwa ni mkakati wa TASAF wa kuziongezea kaya maskini kipato kwa kukidhi mahitaji muhimu hususani katika Nyanja za elimu,afya,lishe na uchumi, ambapo kwa mujibu wa utaratibu asilimia 75 ya fedha ni malipo kwa walengwa wakati asilimia 25 ni kwa ajili ununuzi wa vifaa .

Mpango wa ajira za muda utatekelezwa nchini kote wakati wa kipindi cha hari au kipindi kigumu kama wakati wa ukame au mafuriko kupitia Mpango wa Kunusuru kaya maskini,PSSN ambao umebuniwa na serikali kupitia Mfuko wa Maendeleo ya Jamii TASAF na unatarajiwa kuhudumia kaya maskini zipatazo laki tisa na ishirini elfu nchini kote kazi ianayotarajiwa kukamilika ifikapo mwezi Marchi 2015.

ifuatazo ni picha za baadhi ya wananchi wa shehia ya Mpapa mkoa wa Kusini Unguja wakishiriki katika kazi ya kuchimba mtaro wa maji kupitia utaratibu wa ajira za muda. Baadhi ya walengwa wa Mpango wa kunusuru kaya maskini katika shehia ya Mpapa mkoa wa Kusini Unguja wakishiriki katika kazi ya uchimbaji wa mtaro wa maji kupitia Mpango wa ajira za muda ambao huwawezesha walengwa kulipwa fedha . Mtaro wa maji uliochimbwa na walengwa wa Mpango wa kunusuru kaya maskini katika shehia ya Mpapa wilaya ya Kusini Unguja inayotekelezwa chini ya mpango wa ajira za muda kupitia TASAF.
Mmoja wa walengwa wa Mpango wa kunusuru kaya maskini wa TASAF katika shehia ya Mpapa wilaya ya Kati Mkoa wa kusini Unguja akishiriki kazi ya kuchimba mtaro wa maji.

Lazima;Hatua zaidi zatakiwa kuchukuliwa wahusika wa ESCROW.

Wakati baadhi ya wananchi na taasisi mbalimbali nchini zikiendelea kushinikiza uwajibishwaji wa baadhi ya viongozi waliohusika na wizi kwenye akaunti ya Tegeta Escrow, umoja wa shirikisho la chuo kikuu cha Dodoma umeshauri hatua zaidi zichukuliwe dhidi ya wahusika wote kwani kuvuliwa nyadhifa zao pekee haitoshi. 


Aidha shirikisho hilo limempongeza Rais Jakaya Kikwete kwa kuanza kuwawajibisha baadhi yao likimshauri kuendelea pia kuwashughulikia wale wote waliobaki katika sakata hilo.

Tamko hilo lililotolewa mjini Dodoma na Rais wa shirikisho hilo Fredrick Luterano limedai kuwa mazoea yaliyojengeka hapa nchini kwa baadhi ya viongozi kuvuliwa nyadhifa zao bila hatua zaidi kuchukuliwa umekwisha na sasa umefika muda wa kuchukua hatua zaidi ili liwe fundisho kwa wengine. 


Kwa upande mwingine Rais huyo wa shirikisho la chuo kikuu cha Dodoma akatumia nafasi hiyo kuzitaka mamlaka za vyama vya siasa kuwachukulia hatua wanachama wao wanaopita mitaani wakigawa fedha na kutangaza nia ya kugombea nyadhifa mbalimbali za uongozi ikiwemo Urais.

Sakata la wizi wa fedha za akaunti ya Tegeta Escrow limechangia kujiuzuru kwa mwanasheria mkuu wa Serikali Jaji Fredrick Werema na Waziri wa Ardhi, Nyumba na maendeleo ya Makazi Profesa Anna Tibaiujka akitakiwa kujipima ambapo Katibu mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini Eliakimu Maswi akisimamishwa kupisha uchunguzi na Waziri wa Nishati na Madini Profesa Sospeter Mhongo akiwekwa kiporo.

Zachembe!!!!!!!!! WELLU ANASA MIMBA TENA!



Msanii wa filamu Bongo, Wellu Sengo, ‘Matilda’.

IMEVUJA! Msanii wa filamu Bongo, Wellu Sengo, ‘Matilda’, licha ya kuwa na mtoto mdogo ambaye hajafikisha hata mwaka, inadaiwa tayari amenasa ujauzito mwingine.Chanzo makini kinaeleza kuwa ujauzito huo ni wa mmoja wa wasanii wenye majina maarufu hapa nchini, ambao wamekuwa katika uhusiano kwa muda mrefu sasa.

Katika mawasiliano kwa njia ya simu, Wellu baada ya kubabaika, alikiri kuwa na ujauzito na kumtaja msanii huyo kama ndiye mwenye mzigo, lakini jina lake linahifadhiwa kwa sasa kwa vile mwenyewe hakupatikana ili kuzungumzia madai hayo.

“Haa, wewe nani kakuambia habari hizi, lakini aah, ni kweli bwana nina ujauzito na mwenyewe ni (anamtaja jina). Si unajua tena mambo ya kawaida haya,” alisema muigizaji huyo. 


Msanii huyo anayetajwa kuhusika na jambo hilo, ambaye hata hivyo ni mume wa mtu, amekuwa akionekana kuwa Wellu karibu katika maeneo mengi ya starehe na kijamii akiwa. Baadhi ya wasanii wamekuwa wakimdhihaki mwanaume huyo kwa kumuona kuwa haendani kimuonekano na mwanadada huyo.



GPL

JOKATE ASAPRAIZIWA NA MILLEN MAGESE

 
Mwanamitindo maarufu Bongo, ambaye anafanya kazi zake nje ya nchi Happyness Magesse ‘Millen’.


Mwanamitindo maarufu Bongo, ambaye anafanya kazi zake nje ya nchi Happyness Magesse ‘Millen’ ambaye pia alishawahi kunyakua taji la Miss Tanzania 2001, ‘amemsapraiz’ mwanamitindo na mbunifu Jokate Mwegelo, kwa kumpatia keki yenye sura ya mdomo wake. 

Awali, kulikuwa na kikao cha kawaida cha kujadili mambo mbalimbali ya kikazi baina yao kilichofanyika ndani ya hoteli ya Hyatt Kempisky, iliyopo Posta Jijini Dar, lakini kumbe Millen alikuwa ameandaa keki. 


 
Mwanamitindo na mbunifu Jokate Mwegelo.

“Yaani mimi nilijua tunakutana kama tulivyopanga, lakini cha kushangaza nikakuta watu wakiongozwa na dada yangu Millen wameniandalia keki mbalimbali ikiwemo moja kama mdomo wangu kabisa na kidoti juu,
 
 kwa kweli nilifurahi sana siwezi kuelezea,” alisema Jokate.

Maajabu;Mtoto wa miaka 2 aua mama yake

Maafisa nchini Marekani wanasema kuwa mtoto mmoja mdogo mvulana wa miaka miwili amempiga risasi kimakosa mama yake mzazi na kumuua ndani ya duka moja kubwa la uuzaji bidhaa la Wal-Mart.


Maafisa wa usalama wanasema bunduki iliyotumika iliyokuwa imefichwa ilichomoka wakati mvulana huyo alipokaribia na kuligusa begi la mkononi la mama yake mwenye umri wa miaka 29.

Tukio hilo limetokea katika mji wa Hayden, katika jimbo la Idaho.Msemaji wa Kaunti hiyo anasema mwanamke huyo alikuwa na kibali cha kumiliki

Ni sheeeeeeeeeda!!!!!!!!!!! RAYUU AMUANIKA MWANDANI WAKE

 
Msanii wa filamu Bongo, Alice Bagenzi ‘Rayuu’.


MSANII wa filamu Bongo, Alice Bagenzi ‘Rayuu’ amezua gumzo baada ya picha zake zinazomuonesha akiwa chumbani na mwanaume kuenea mtandaoni, huku kijana huyo akionekana kujichora tatoo yenye jina la mwanadada huyo. 




Kijana huyo aliyefahamika kwa jina moja la Brown hakuweza kupatikana ili kuthibitisha uhusiano wake na mrembo huyo, lakini Rayuu alikiri kuwa ingawa picha iliyowekwa mtandaoni ilionyesha wakiwa kikazi zaidi, huyo ni mpenzi wake wa siku nyingi. 




“Hizo picha ni sehemu ya vipande vya kwenye wimbo wa huyo mwanaume, ukweli ni mpenzi wangu wa siku nyingi na anataka kunioa, ndiyo maana kafikia hatua ya kujichora jina langu, sina kipingamizi, tunaomba Mungu atufanikishe tufunge ndoa,” alisema.
 GPL
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...