2015-03-31

Ni shiiiiiiiiiiiidah!!!!!!!!!!!!! ALI KIBA AAHIDI KUWACHEKETUA MASHABIKI WAKE

Meneja Mkuu wa Global Publishers, Abdallah Mrisho (W) akiongea na waandishi wa habari katika Hoteli ya Atriums kuhusiana na shoo ya Pasaka Dar Live. 


Wandishi wa habari mbalimbali wakiwa kazini kama inavyoonekana. 


Kiongozi wa kundi la sarakasi la Masai Warrios akiongea jambo kuhusu shoo hiyo siku ya Pasaka Dar Live. 

Meneja Uhusiano wa Vodacom Tanzania, Matina Nkurlu akielezea jinsi Vodacom Tanzania ambao ndiyo wadhamini wakuu wa shoo hiyo walivyojipanga. 


Mwakilishi wa Kinywaji cha Vita Malt, Bahati Sindi akiongea kuhusiana na shoo hiyo itakayolitikisa jiji la Dar na vitongoji vyake. 


Msaga Sumu akihojiwa na waandishi wa habari. 

Kutoka kushoto, Kiongozi wa MC Darada, Bahati Sindi pamoja na Msaga Sumu katika picha ya pamoja. 


10 Wasanii watakaotumbuiza Pasaka Dar Live wakiwa katika picha ya pamoja ndani ya Hoteli ya Atriums jijini Dar. 


11 Kiongozi wa Mashauzi Classic, Isha Mashauzi akihojiwa na mwandishi. 


Msanii wa kizazi kipya anayetamba na wimbo wa Chekecha Cheketua, Ali Saleh ‘Kiba’ (katikati) akielezea alivyojipanga kutoa burudani ya nguvu katika shoo yake ya Mwana Dar Live itakayofanyika Sikukuu ya Pasaka. 


kutoka kushoto, mwakilishi wa Kampuni ya Vinywaji vya Vita Malt, Bahati Sindi akiwa na Isha Mashauzi pamoja na Msaga Sumu katika picha ya pamoja. 


Mwakilishi wa Vodacom, Martina Nkuyu akiongea na Msaga Sumu kama wanavyoonekana.

MSANII wa kizazi kipya anayetamba na wimbo wa Chekecha Cheketua, Ali Saleh ‘Kiba’ ametamka kuwa amejipanga vya kutosha anahakikisha anawapagaiwisha mashabiki wake wataojitokeza katika shoo ya Mwana Dar Live siku ya Sikukuu ya Pasaka, Aprili 5 mwaka huu katika Ukumbi wa Taifa wa Burudani, Dar Live, Mbagala.

Akizungumza na waandishi wa habari leo katika Hoteli ya The Atriums jijini Dar, Kiba alisema amejipanga vya kutosha kuhakikisha anadondosha bonge la burudani kwa mashabiki wake wataokuja katika shoo hiyo ambapo siku hiyo ataupiga wimbo huo wa Chekecha Cheketua kwa kutumia ‘live’ bendi.

“Nawaomba mashabiki wangu waje kwa wingi kwani siku hiyo nimejipanga vya kutosha kuhakikisha napiga shoo kali ambayo itawapagawisha watu wote ambao watakuja ukumbini hapo ambapo nyimbo zote nitaziimba kwa kutumia vyombo vya jukwaani ‘live band’ .

Naye Mratibu wa Burudani katika Ukumbi huo wa Dar Live, Abdallah Mrisho ‘Abby Cool’ amewataka mashabiki wote wapenda burudani wasikose kufika katika ukumbi huo siku hiyo ya Sikukuu ya Pasaka kwani watapata furaha ya kufika ukumbini hapo.

Pia, Isha Mashauzi na Mashauzi Classic pamoja na Msaga Sumu na Masai Warriors watanogesha burudani mbalimbali katika siku hiyo wakimsindikiza Ali Kiba.

Je,ni Sahihi Mkuu wa Wilaya, Paul Makonda Kutaka Kumhoji Gwajima Wakati Polisi Walishamhoji ???...Haya Ni Maoni Ya Malisa Na Mtatiro Kuhusiana na Sakata Hili


Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Paul Makonda ambaye alikuwa amemwandikia Gwajima barua akimwita ofisi kwake, jana mchana alimtembelea hospitalini hapo kwa ajili ya kumjulia hali kiongozi huyo lakini akasisitiza kuwa nia yake bado ipo palepale.

“Nilimtaka leo aripoti ofisini kwangu lakini kwa bahati mbaya anaugua na amelazwa. Nitakwenda kumuona ili nijue hali yake ikoje,” alisema Makonda kabla ya kufunga safari kwenda hospitali alikolazwa.

Alisema pia atataka kiongozi huyo wa kiroho amweleze anavyoelewa maana ya uhuru wa kuabudu unaoelezwa katika Katiba, usajili wa taasisi yake na katiba ya taasisi hiyo.

“Mimi ni mwenyekiti wa Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Wilaya ya Kinondoni. Niliagiza polisi wamkamate na baadaye wakimaliza kumhoji aje kwangu pia atahojiwa na jopo la watu 20,” alisema Makonda.

Baada ya kauli hiyo, mijadala kadhaa iliendelea katika mitandao ya kijamii hususani Facebook na Twitter ambapo baadhi ya wananchi walitoa maoni yao wakishangaa na kuhoji uhalali wa DC kutaka kuhoji masuala ambayo yako chini ya mamlaka nyingine kisheria. Yafuatayo ni moja ya maoni hayo yaliyoandikwa kwenye kurasa zao za Facebook.

JULIUS MTATIRO...


YA GWAJIMA vs PENGO
“Polisi wanamuhoji mtuhumiwa ili waone kama ana kosa la kumshitaki au la, hapohapo Mkuu wa Wilaya husika naye anamuandikia barua kumtaka aripoti kuhojiwa na Mkuu wa Wilaya.

"Hakuna Sheria wala Kanuni inayompa mamlaka Mkuu wa Wilaya kujihusisha na upepelezi au ufuatiliaji wa makosa ya jinai. Ni kupoteza muda tu kwa wakuu wa wilaya wanapojaribu kuwaita watuhumiwa wakawahoji, labda pia ni kutojua nini kimewaweka kwenye zile ofisi.

"Pamoja na mimi kutokukubaliana na ujengaji hoja wa matusi uliotumiwa na Mchungaji GWAJIMA kumfikishia ujumbe Kadinali Pengo, namshauri Gwajima asiitikie wito huu wa rafiki yangu, mdogo wangu na kijana mwenzangu DC wa Kinondoni, PAUL MAKONDA, na DC hatakuwa na cha kufanya.

"Wakuu wa wilaya wanahitaji mafunzo zaidi juu ya kazi yao vinginevyo nyadhifa hizi zifutwe tubaki na wakuu wa mikoa na wakurugenzi wa halmashauri. Kwa sababu wakuu wa wilaya wamekosa kazi, sasa wameanza kujishughulisha na upepelezi wa makosa ya jinai. Sina mbavu hapa....”

GODLISTEN J MALISA...


MAKONDA ACHANA NA GWAJIMA, SHUGHULIKA NA YANAYOKUHUSU.!
“Nimecheka sana baada ya kuamka na kukuta Habari kwenye media kuwa eti Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Ndg.Paul Makonda amemtaka Askofu Gwajima akaripoti kwake haraka iwezekanavyo mara tu baada ya kutoka Hospitali kwa ajili ya mahojiano.

"Hahahaah hiki ni kituko cha mwaka. Mahojiano gani Makonda anataka kumfanyia Askofu Gwajima? Kwamba Makonda nae amekuwa Afisa Upelelezi wa jeshi la Polisi au?
"Navyoelewa ni kuwa swala la Gwajima ni Criminal Defamation. Ndio maana Jamhuri ikaingilia suala hilo. Na kwa utaratibu wa criminal case ni kuwa Polisi wanafanya upelelezi wao then State Prosecutor anasimama mahakamani dhidi ya mtuhumiwa.

"Sheria zote na machapisho yote ya kisheria yanazohusika na Defamation cases kwa nchi yetu (Defamation Law in Tanzania; Leading Statutes, Cases &Materials) hakuna hata moja inayotoa mandate kwa Mkuu wa Wilaya kufanya upelelezi au kuhoji.

"Sheria ya Kanuni za Adhabu Tanzania (Penal Code) haitoa mandate hiyo. Wala sheria ya Magazeti (Newspapers Act, 1976), wala sheria ya utangazaji (Broadicasting services Act, 1993, wala sheria ya mwenendo wa makosa ya madai (Civil Procedure Code, 1966) wala Sheria ya Ushahidi (The Tanzania Evidence Act, 1966).

"Hizi zote ni sheria zinazodeal na defamation na hakuna hata moja iliyogrant mandate kwa mkuu wa wilaya kuhoji wala kupeleleza. Wala hakuna sheria kati ya hizo nilizozitaja inayosema "Polisi wakishafanya upelelezi Mkuu wa wilaya amuite mlalamikiwa ili ajiridhishe"

"Sasa najiuliza logic ya Makonda kumuita Gwajima kwa mahojiano ni nini? Kwamba anadhani yeye ana nguvu kuliko Polisi? Kwamba anadhani Polisi hawawezi kufanya upelelezi kwa ustadi mkubwa kama yeye? Kwamba haamini upelelezi unaofanywa na jeshi la Polisi?

"Kweli ujinga ni kipaji. Yani kabla hata Polisi hawajamaliza upelezi wao wewe ushakurupuka unataka Gwajima akuone? Akuone ili iweje? Kama ni kuhojiwa ameshahojiwa na Polisi na kama atapatikana na kesi ya kujibu atapelekwa Mahakamani. Sasa wewe unataka akuone ili iweje? Aje akuombee toba au? 


"Nadhani Polisi wamzuie huyu "DC wa miezi 6", maana anaweza kuharibu upelelezi unaoendelea kwa kutafuta "cheap popularity".

"Sijawahi kusikia popote duniani, DC anaingilia kesi ambayo upelelezi wake haujakamilika. Hata upelelezi ukikamilika kesi haipelekwi kwa DC inapelekwa mahakamani. Sasa huyu Makonda kapata wapi "kiherehere" cha kumuita Askofu Gwajima.

"Au labda anataka kutubu? Lakini hata kama anataka kutubu angesubiri kwanza Gwajima atoke hospitali, kisha amuite waongee. Sio kuandika mitandaoni na kutangaza kwenye vyombo vya habari eti Gwajima akitoka amuone.

"Gwajima yupo ICU, wewe unatangaza kwenye media eti akitoka akuone.. hii ni akili au matope? Unadhani huko ICU Gwajima anasoma blogu na kusikiliza "Radio Mbao" kama ulivyozitumia kutoa agizo lako? Acha "akili ndogo" kijana.!

"Wakati fulani Mwenyekiti wa CHADEMA Mhe.Freeman Mbowe aliwahi kusema wakuu wa wilaya hawana kazi ndio maana muda mwingi wanatumika kisiasa au kuingilia mambo yasiyowahusu. Mbowe alisema wakuu wa wilaya wana kazi mbili tu kubwa "Kufungisha ndoa na kuandaa vyeti vya vizazi na vifo."

"Hii ya vizazi na vifo kwa sasa inafanywa na RITA, so kwa mujibu wa Mbowe wakuu wa wilaya wamebaki na kazi moja kubwa ambayo ni KUFUNGISHA NDOA .

"Sasa najiuliza hivi Kinondoni hakuna watu wanaofunga tena ndoa zao Bomani ili Mkuu wa wilaya apate kazi za kufanya? Maana Makonda anaonekana hana kazi ndio maana anaanza kuingilia hadi mambo ya kisheria ambayo hayajui kabisa.

"Yani kwenye sheria "this guy is typical tabularasa/layman" Nashauri kama Makonda hana kazi ya kufanya ashughulike na usafi wa mazingira maana manispaa ya Kinondoni bado usafi hauridhishi, asimamie halmashauri izibue mitaro ya maji taka, na kuzuia manyanyaso kwa wafanyabiadhara wadogo.

"Haya masuala ya kisheria aachane nayo maana hayamhusu kabisa na hayawezi.! Wasalaam,”

Ufafanuzi wa Tukio la Kula Njama na Kujaribu Kumtorosha Askofu Josephat Gwajima Akiwa Hospitali.....


Tarehe 30/03/2015 waandishi wa habari walifika kituo Kikuu cha Polisi wakitaka kujua uhalali wa silaha iliyokamatwa tarehe 29/03/2015. Silaha hiyo ni Bastola aina ya BERRETA yenye namba CAT5802 ikiwa na risasi tatu. Pia zilikamatwa risasi 17 za Short Gun.

Ufafanuzu ni kama ifuatavyo:


Uchunguzi wa kina na wa kitaalam sasa umethibitisha kwamba silaha hiyo inamilikiwa kihalali na Askofu Josephat Gwajima. Kuhusu risasi 17 za Short Gun ni kwamba Askofu Gwajima anamiliki Bunduki aina ya Short Gun yenye namba 102837 ambayo inatumia risasi za aina hizo zilizokamatwa.

Kuhusu watu 15 wanaotuhumiwa kujaribu kumtorosha Askofu Josephat Gwajima bado uchunguzi unaendelea. Aidha watu hao pia wanahojiwa kuhusu suala la kukutwa na silaha na risasi zilizotajwa hapo juu wakati wao sio wamiliki halali za silaha hiyo na risasi hizo na idadi iliyotajwa kwa mujibu wa sheria.

Baada ya uchunguzi wa suala hilo jalada la kesi litapelekwa kwa mwanasheria wa Serikali kabla hawajafikishwa mahakamani ili sheria ichukue mkondo wake.

KAMISHNA WA POLISI KANDA MAALUM,
S. H. KOVA,
DAR ES SALAAM.

Kesi ya Mchungaji Mtikilia Kupinga Mahakama ya Kadhi Imeanza Kuunguruma Mahakamani......Mtikila Anapinga Mahakama hiyo Kujadiliwa Bungeni,Serikali kutoa Majibu Leo Kortini



Mwenyekiti wa Democratic Party (DP), Mchungaji Christopher Mtikila, ameiomba Mahakama Kuu ya Tanzania Kanda ya Dar es Salaam, kutoa amri kwa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, kusitisha kujadili suala lolote linalohusu kuanzishwa kwa Mahakama ya Kadhi.

Mtikila aliwasilisha maombi yake jana mbele ya jopo la majaji watatu likiongozwa na Mwenyekiti, Jaji Richard Mziray, anayesaidiana na Jaji Lawrence Kaduri na Said Kihio.

Kesi ya msingi ambayo Mtikila anaomba Mahakama ya Kadhi isiruhusiwe nchini, ilipangwa kutajwa jana.

Upande wa Jamhuri uliongozwa na Mawakili wa Serikali Wakuu, Gabriel Malata na Kasori Sarakikya, ulidai kuwa utawasilisha majibu ya maombi ya Mtikila leo.

Mtikila alidai kuwa anaomba kuwasilisha hati ya dharura mahakamani akitaka bunge hilo lisijadili wala kuzungumzia suala la Mahakama ya Kadhi.

“Ina maana suala hili baada ya kufunguliwa mahakamani linajadiliwa huko nje ya Mahakama?,” alihoji Jaji Mziray na kuitikiwa na Mtikila. 

Jopo hilo lilisema upande wa Jamhuri uwasilishe majibu ya maombi ya Mtikila kwa njia ya maandishi leo na kesho kesi hiyo itatajwa.

Mtikila alifungua kesi ya madai kupinga kitendo cha serikali kupeleka muswada bungeni wa kutunga sheria ya kuanzishwa kwa Mahakama ya Kadhi, kwamba kuanzishwa kwake ni kinyume cha Katiba ya nchi.

Mtikila ameiomba Mahakama itoe amri kwamba wale walio kwenye mamlaka ya serikali akiwamo Waziri Mkuu, Mizengo Pinda; Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais (Mahusiano na Uratibu), Mary Nagu; Waziri wa Katiba na Sheria, Dk. Asha-Rose Migiro; Mwanasheria Mkuu wa Serikali, George Masaju na Waziri wa Kilimo, Chakula na Ushirika, Stephen Wasira na wenzao, watoe sababu kwa nini wasifungwe kifungo kisichopungua miaka mitano ikiwa watashindwa kujieleza.

Pia, Mtikila kupitia hati yake ya madai iliyopewa usajili namba 14 ya mwaka huu, ameomba Mahakama itoe amri ya vigogo hao kufungwa kifungo hicho kutokana na kuchezea Katiba ambayo ni sheria mama ya nchi. 

Katika hati yake, Mtikila pia anaiomba Mahakama itoe amri kwamba Mahakama ya Kadhi na Jumuia ya Kimataifa ya Kiislamu (OIC), itangaze kuwa ni haramu kwenye ardhi ya Tanzania.

Pamoja na mambo mengine, Mtikila anadai kuwa suala la serikali kuandaa Muswada wa Kiislamu na kuuwasilisha bungeni na kitendo cha Bunge kukubali zaidi ya kuukataa ni sawa na uhaini, kinachofanywa na waliopanga kuupeleka muswada huo bungeni.

Anaendelea kudai kuwa kitendo hicho ni sawa na uvunjifu mkubwa wa viapo vya viongozi hao walivyoapa wakati wa kushika nafasi za uongozi wa umma na ni kinyume cha kifungu cha 19 cha Katiba ya nchi kinachoeleza kwamba masuala ya dini na kuabudu yatakuwa ni ya mtu binafsi na kuongeza kuwa uendeshaji wa mambo au taasisi za kidini hazitakuwa sehemu ya mamlaka ya nchi.

Profesa Lipumba na Dr. Slaa Wamjulia Hali Gwajima......Walitupia Lawama Jeshi la Polisi.


Mwenyekiti wa Chama cha Wananchi (CUF), Prof. Ibrahim Lipumba, jana alimtembea Askofu Gwajima hospitalini hapo kumjulia hali.

Lipumba amekuwa kiongozi wa pili wa kisiasa kufika hospitalini hapo kumjulia hali Gwajima, baada ya Katibu Mkuu wa Chadema, Dk Willibrod Slaa aliyefika kwa mara ya kwanza Jumamosi na kurudi tena jana.

Profesa Lipumba ambaye hivi karibuni pia aliishiwa nguvu wakati akihojiwa na polisi, alisema kitendo kinachofanywa na jeshi hilo cha kutumia nguvu kinatakiwa kukemewa kwa nguvu zote. 


Akizungumza baada ya kumjulia hali Gwajima, alisema yeye ni miongoni mwa waliopatwa na hali hiyo akiwa mikononi mwa polisi kutokana na kuacha kuuliza suala husika na kutishatisha, kusumbua sumbua, kitu kinachomfanya anayehojiwa kujisikia vibaya na hata kupoteza fahamu.

Aliongeza kwamba kwa kuwa Kardinali Pengo ameshatangaza msamaha kwa Askofu Gwajima, hakuna haja ya kuendelea kumshikilia.

Dk Slaa alisema kinachofanywa na polisi ni upotoshaji na hapingi wala haingilii kinachoendelea kati ya Gwajima na Pengo, bali analaani kitendo cha polisi kupotosha ukweli.


Dk Slaa alisema polisi wanapotosha ukweli kwa kuwaeleza wananchi kitu ambacho hakina ukweli kwa masilahi yao kama ambavyo wamekuwa wakiwafanyia viongozi wa siasa, akiwamo yeye. 

Alisema kitendo kilichomkuta Gwajima hata yeye kiliwahi kumkuta .Alikamatwa na bastola aliyoisajili na kuilipia kila kitu, siku iliyofuata polisi wakamtuhumu kuwa ni jambazi anamiliki silaha isivyo halali.

“Mimi nasema waache wawapeleke mahakamani, ukweli utabainika,” alisema Slaa.

Sakata la Dr. Slaa Kutaka kuuawa: Mke Wake Ahojiwa Polisi Kwa Masaa Matatu.


Mke wa Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Dk. Willibrod Slaa, Josephine Mushumbusi, jana alitoa ushahidi katika Kituo Kikuu cha Polisi jijini Dar es Salaam, kuhusiana na tuhuma zinazomkabili Khalid Kagenzi, za kutaka kumdhuru mumewe.

Kutokana na hatua hiyo ya Mushumbusi, Dk. Slaa alisema tayari wamefunga ushahidi kwa upande wake. Mushumbusi ambaye aliongozana na mumewe, Dk. Slaa walifika katika kituo hicho saa 4:00 asubuhi na kutoka saa 7:25 mchana.

Akizungumza na waandishi wa habari baadaye, Dk. Slaa alisema alimsindikiza mkewe kituoni hapo kutoa maelezo akiwa shahidi yake.

“Leo mke wangu alikuja kutoa ushahidi. Na maelezo yote aliyoyatoa yameandikwa. Ameyapitia na mimi nimeyapitia. Hivyo, kwa upande wangu ushahidi nimekamilisha. Imebaki kwao tu kwa hatua zaidi pamoja na faili letu kupelekwa kwa Mkurugenzi wa Mashitaka (DPP),” alisema Dk. Slaa.

Aliongeza: “Ninaomba ieleweke kwamba mke wangu ni shahidi na siyo mtuhumiwa kama ambavyo nimekwisha kueleza. Naomba msipotoshe kama ilivyotokea awali.”

Kwa upande wake, Mushumbuzi alisema wakati tukio linatokea, alishindwa kutoa ushahidi alipoitwa na Jeshi la Polisi kwa sababu alikuwa safarini, lakini baada ya kurudi alitoa taarifa kwa jeshi hilo.

“Wakati tukio linatokea, niliitwa kutoa ushahidi wangu, lakini sikufanya hivyo kwa sababu nilikuwa safari. Niliporudi niliwaambia, kwa hiyo wakaniambia nije leo,” alisema Mushumbusi.

Aliongeza: “Maelezo ambayo nimeyatoa ni yale yale niliyosema kwenye vyombo vya habari. Kwa hiyo yameandikwa na nimeyapitia nikajiridhisha.”

Awali, akizungumza na waandishi wa habari juu ya wito wa mke wa Dk. Slaa, Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Suleiman Kova, alisema hakuwa na taarifa na jambo hilo na kwamba suala hilo linawezekana kwa kuwa ni utaratibu wa kawaida wa utendaji kazi kwa jeshi hilo.

“Sina taarifa juu ya jambo hilo. Lakini hilo ni jambo la kawaida. Siyo jambo kubwa sana na ni utaratibu wa kawaida wa utendaji kazi wa polisi. Na kama amekuja kuhojiwa ni wito, ambao anaweza kuitwa mtu mwingine yeyote,” alisema Kova. 

Katika maelezo yake kwa vyombo vya habari, Mushumbusi alidai alibaini njama za Kagenzi ambaye alikuwa mlinzi wa Dk. Slaa, kutaka kumuua mumewe baada kukutwa na msaidizi wake wa ndani akiwa katika meza ya chakula, ambayo hutumika kwa ajili ya kuandalia chai ya mumewe japokuwa haikuwa kawaida yake kunywa chai katika meza hiyo.

Alisema hata hivyo, baada ya kukutwa na msaidizi wake wa kazi za ndani, Kagenzi alishtuka na kumwaga chai na hata alipoulizwa sababu za kufanya hivyo, hakutoa sababu za msingi.

Taarifa za awali za Kagenzi kutaka kumdhuru Dk. Slaa zilitolewa na Mjumbe wa Kamati Kuu ya Chadema, Mabere Marando, mbele ya waandishi wa habari, ambaye alieleza kuwa amekuwa akitumiwa na maofisa 22 wa vyombo vya usalama katika miaka miwili iliyopita kufanya mipango hiyo dhidi ya chama hicho.

Alidai Kagenzi amekuwa akitumiwa na maofisa usalama wa vyombo hivyo kupata taarifa nyingi za Chadema na kuziwasilisha kwa Chama Cha Mapinduzi (CCM).

Marando alidai mipango hiyo iligunduliwa na kitengo cha usalama cha Chadema kupitia simu za Kagenzi na kwamba, ililenga kuiumiza Chadema kisiasa. 

Alidai katika hujuma hizo, Kagenzi amekuwa akiwasiliana na mmoja wa vigogo wa ngazi ya taifa wa CCM.

Marando alidai kuanzia Desemba, mwaka jana, Kagenzi alikuwa amekwishafadhiliwa Sh. milioni saba kwa ajili ya matumizi ya mawasiliano ya simu kufanikisha upatikanaji wa taarifa za Chadema kupitia vikao vyake mbalimbali ikiwamo Kamati Kuu.

Alidai alipohojiwa na Chama, Kagenzi aliwapa kitabu chake cha kutunza kumbukumbu ambacho kinaonyesha mawasiliano kati yake na baadhi ya maofisa wa vyombo vya usalama aliowataja kwa majina na namba za simu zao za mikononi.

Maaskofu na Wachungaji Watoa Tamko Zito Kuhusiana na Kudhoofu Kwa Afya Ya Gwajima Mikononi mwa Polisi.....Wapanga Kuonana na IGP Mangu. Tamko Liko Hapa.


Sisi maaskofu na wachungaji kutoka makanisa mbalimbali tumeshtushwa na kusikitishwa kwa taarifa ya ugonjwa wa Askofu na mtumishi mwenzetu Josephat Gwajima ambaye tarehe 27/03/2015 alifika kituo cha polisi cha kati kuitikia wito wa polisi uliomtaka kwenda kujibu shutuma za kutumia lugha ya matusi kwa kardinali Pengo.

Tumepata fursa ya kutafakari na kujadili kwa kina hali iliyompata Askofu mwenzetu hasa baada ya kuzingatia kuwa Askofu Gwajima alifika polisi akiwa mzima na mwenye afya njema lakini wakati wa akihojiwa na polisi, hali yake ilibadilika ghafla kiasi cha kupelekea yeye kulazwa hospitali ya TMJ akiugua tena kwenye wodi ya wagonjwa mahututi yaani (ICU) katika chumba cha uangalizi maalum.

Maswali yetu makuu ni kitu gani kimempata mwenzetu? Tunajiuliza, je vyombo vya usalama vimekua sio sehemu salama kama zamani?

Tukiwa bado tunatafakari hill, tumeshtushwa tena baada ya kupata taarifa ya kuwa Wachungaji Wasaidizi wa Askofu Gwajima pamoja na walinzi wake waliokuwepo hospitalini hapo kwa ajili ya kumuuguza nao pia wamekamatwa kwa tuhuma za kutaka kumtorosha Askofu Gwajima.

Jambo hili linashangaza zaidi maana wachungaji wale wale waliokuwa naye akiwa mzima wa afya wakati anaelekea polisi ndio wale wale wanatuhumiwa kutaka kumtorosha akiwa mgonjwa.

Ni jambo la kushangaza na lisiloingia akilini kuwa wasaidizi hao wa Gwajima walitaka kumtorosha wakati Gwajima kama angekua na nia hiyo angekwisha fanya hivyo mana alikuwa na uwezo wa kutoroka alipokua Arusha kwenye kikao cha Maaskofu wakuu wa makanisa ya Kipentekoste ambao alipata taarifa za kuitwa Polisi. 

Isitoshe Gwajima aliitikia wito na kwenda polisi mwenyewe kwa miguu yake bila kushurutishwa, wala hakufikishwa polisi kwa nguvu.

Swali: Kama alikua anaona ugumu wa kutoroka wakati hakuna polisi anayemlinda na huku akiwa mwenye afya tele, itakuaje rahisi kutoroshwa leo akiwa mahututi na akiwa kwenye ulinzi mkali wa polisi? Mbona hii inastaajabisha?

Jambo jingine linalotupa shida ni kuhusu mlalamikaji wa kesi hii inayomkabili Askofu Gwajima. Tumeelezwa na wasaidizi wa Askofu Gwajima kuwa pale polisi walielezwa kuwa aliyefungua kesi hii sio Pengo ila mtu mmoja aitwaye Aboubakar.

Kwa ufahamu wetu juu ya sheria unatutuma kuamini kuwa Aboubakar sio MTU sahihi wa kufungua kesi hiyo sababu hawezi kutuonyesha ameumizwa kiasi gani na matamshi ya Askofu Gwajima.

Isitoshe, Kardinali Pengo mwenyewe ametamka katika Ibada yake ya Jumapili hii ya tarehe 29/03/2015 kuwa amemsamehe Gwajima, yupi tena mwenye uchungu wa kumzidi Kardinali Pengo? 

RAI YETU:
Rai yetu ni kwamba, ni vizuri serikali pamoja na vyombo vyake vya usalama vikatumia weledi katika kushughulikia mambo ya kidini na viongozi wake kwani yanaweza kusababisha chuki dhidi ya serikali na pia kupelekea mpasuko mkubwa wa kidini katika jamii yetu iliyo na historia nzuri ya umoja na mshikamano na ushirikiano katika matukio yote ya kimaisha.

Tunaomba serikali isaidie kuondoa mkanganyiko huu na busara kubwa itumike ili kuepusha uvunjifu wa Amani katika jamii.

MAAMUZI YETU:
Jambo hili linazungumzika, maana hata hivyo tumeshaazimia kukutana na IGP ili kupata suluhisho juu ya jambo hili.

Kwa niaba ya maaskofu na wachungaji:
Mwenyekiti: Askofu Dr. Mgullu Kilimba
Katibu: Askofu Dr. Dramas Mukassa

Sad Newzzzzzzzz:MAITI YAPATA AJALI WAKATI IKIEDA KUZIKWA

  Hii story iko kwenye Headlines Indonesia.. Ilikuwa ni msiba wa mtu mmoja ambapo wakiwa njiani kwenda kwenye mazishi likatokea tukio jingine, story ikawa kubwa zaidi. 

Waombolezaji walikuwa wamebeba mwili wa marehemu kwenda makaburini kwa ajili ya mazishi, mwili wa marehemu uliokuwa umebebwa ulidondoka bila wao kujua na kuendelea na safari.. watu waliokuwa nyuma yao wakaona mwili huo katikati ya barabara. 

Ilibidi wawaite na kuwaambia kwamba mwili wa marehemu walikuwa wameuacha nyuma yao, wakarudi kuuchukua na kuurudishia ndani ya jeneza na kuendelea na safari ya kwenda kuzika. 

Video ya tukio hilo iliyowekwa katika mtandao imeshaangaliwa na watu zaidi ya 110,000 ndani ya siku mbili.
Bonyeza play hapa chini kuangalia tukio hilo…

HIZI NDIO SURA MBILI ZA ASKOFU GWAJIMA!............soma hapa


SIKU chache baada ya Askofu wa Kanisa la Ufufuo na Uzima, Josephat Gwajima kukamatwa na kuhojiwa na polisi na hatimaye kuzimia, utata mpya umeibuka juu ya kiongozi huyo wa kiroho. 

Utata huo unahusu uraia, historia yake, utajiri na umiliki wa silaha ambayo Jeshi la Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam linadai haina kibali huku yeye akidai ana vibali vyote.
Hali hiyo imeibuka huku nyuma ya pazia kukiwa na sintofahamu juu ya hatima yake. 

Ingawa Askofu Gwajima, amelazwa Hospitali ya TMJ kwa siku ya tano leo, bado anaendelea kushikiliwa na polisi kwa tuhuma za kutoa lugha chafu dhidi ya Askofu wa Kanisa Katoliki Jimbo Kuu la Dar es Salaam, Mwadhama Polycarp Kardinali Pengo.

AHOJIWA KWA STAILI YA FBI
Baada ya kujisalimisha polisi Machi 27, mwaka huu, Askofu Gwajima anadaiwa kuhojiwa kwa staili ya Shirika la Upelelezi la Marekani (FBI). 

Inaelezwa alihojiwa na makachero tofauti waliokuwa wakipishana katika chumba cha mahojiano na ambao wanaonekana kubobea katika taaluma hiyo. 

Wakati akidhani mahojiano yamemalizika, inadaiwa waliingia maofisa wengine kumhoji maswali tofauti tofauti, mtindo ambao unatumiwa zaidi na wapelelezi wa FBI. 

Hatua hiyo, pia inadaiwa kuchangia kuzimia kwake ambapo awali alidhani mahojiano yangekuwa ni kuhusu kumkashifu Kardinali Pengo tu.

KULAZWA HOSPITALI
Kabla ya kulazwa katika Hospitali ya TMJ, Askofu Gwajima alipelekwa katika Hospitali ya Polisi Kurasini na baadaye Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) ambapo yeye na wafuasi wake waligoma na kutaka atibiwe TMJ ambapo kuna daktari wake maalumu. 


URAFIKI NA WANASIASA
Askofu Gwajima, kwa muda sasa amekuwa rafiki wa wanasiasa mbalimbali nchini wakiwamo wa vyama vya upinzani, chama tawala, wastaafu pamoja na baadhi ya mawaziri walioko ndani ya Serikali ambao hukutana faragha, hadharani na wengine hushiriki katika ibada kanisani kwake.
Baadhi ya wanasiasa wa upinzani tayari wamemtembelea hospitalini alikolazwa.

UTATA SAKATA LA DK. ULIMBOKA
Sura ya pili ya Askofu Gwajima, ilianza kuonekana mwaka 2012, baada ya kanisa lake kuingia katika utata na sintofahamu baada ya kijana aliyedaiwa kumteka na kumtesa, Mwenyekiti wa Jumuiya ya Madaktari Tanzania, Dk. Steven Ulimboka kukamatwa na polisi. 

Polisi walimkamata kijana huyo kwa kile kilichodaiwa kujisalimisha kwenye kanisa la Askofu Gwajima ambalo alikwenda kutubu kosa la kumshambulia Dk. Ulimboka. 

Mtuhumiwa huyo, Joshua Mlundi, raia wa Kenya alikiri kuhusika kumteka na kumtesa Dk. Ulimboka akiwa na wenzake 12 waliokodiwa na mtu aliyehisi anatoka serikalini. 

Hata hivyo, Askofu Gwajima alisema Mlundi hakwenda kanisani hapo kutubu, bali alitaka kumuona kiongozi huyo wa kiroho baada ya kumweleza kuwa alikuwa na tatizo la kuropoka.

MAISHA YA KITAJIRI
Askofu Gwajima ni kiongozi wa kiroho mwenye ukwasi pengine kuliko wote nchini. 

Anadaiwa anamiliki helikopta yake mwenyewe, gari la kifahari aina ya Hummer lenye thamani ya Sh milioni 250 na nyumba ya ghorofa nne maeneo ya Mbezi Beach, jijini Dar es Salaam. 

Pamoja na kumiliki vitu hivyo, Askofu Gwajima amewanunulia wachungaji wake magari 30, kila mmoja gari zuri la kutembelea wakati wa kueneza injili. 

Pia, amewanunulia waumini wake mabasi 20 ya kuwapeleka kanisani na kuwarudisha makwao siku za ibada na wakati wa maombi maalumu. 

Pia anamiliki shamba la mifugo wilayani Sengerema mkoani Mwanza. 

Katika kanisa lake, Askofu Gwajima amefunga spika maalumu zenye nembo ya ‘JG’ yaani Josephat Gwajima ambazo amezinunua nchini Marekani kwa oda maalumu.

KAULI TATA ZA GWAJIMA
Mwaka jana wakati wa mlipuko wa ugonjwa wa Dengue, Askofu Gwajima alikaririwa akisema hakuna ugonjwa kama huo isipokuwa umetengenezwa ili watu wajipatie fungu kutoka serikalini. 

Alisema mbu aina ya Ades anayeeneza ugonjwa huo, alikuwapo tangu siku nyingi lakini hakuwa na madhara hadi baadhi ya viongozi ambao hakuwataja walipoutangaza na kuwalipa watu ili watangaze wameambukizwa ugonjwa huo.

URAIA NA HISTORIA YAKE
Suala la uraia wa Askofu Gwajima limekuwa mjadala kwa baadhi ya Watanzania, wakionyesha shauku ya kutaka kujua historia ya maisha yake. 

Vyanzo mbalimbali ikiwamo mitandao ya kijamiii ya ‘twitter’, ‘facebook’ na tovuti yake, vimebainisha kuwapo kwa sintofahamu nyingi kuhusu asili yake. 

Katika tovuti yake, Askofu Gwajima ambaye alianzisha kanisa lake mwaka 1994, hakutaja jina la kijiji alichozaliwa ingawa anasema alizaliwa mwaka 1970 mkoani Mwanza. 

Katika tovuti yake hiyo, ameelezea historia yake akisema ni mtoto wa 12 katika familia yao ambayo iliishi katika kijiji ambacho hakikuwa na kanisa. 

Anasema katika tovuti yake kuwa alipatwa na maradhi ya kupooza akiwa na umri wa miaka 10. 

Alitaja sababu iliyosababisha apooze kuwa ni ajali ambayo hakuibainisha ni ya aina gani, ingawa anasema alikaa kitandani kwa muda wa miaka sita na kupoteza matumaini ya kupona. 

Hali hiyo, anaelezea ilisababisha madaktari wathibitishe kuwa asingeweza kurejea katika hali yake ya kawaida, lakini alipona baada ya kutokewa na Yesu na kumponya hali iliyomfanya ampe maisha yake kuanzia siku hiyo. 

Kuhusu elimu yake, askofu huyo anasema amesomea masuala ya Biblia jijini Nairobi nchini Kenya katika shule ya East Africa Pastorial Theological. Hata hivyo, hajaeleza kiwango chake cha elimu alichopata. 

Baada ya kuhitimu alianza kufanya kazi ya kumtumikia Mungu ambapo alifungua kanisa katika Jiji la Mwanza, mji mdogo wa Mugumu uliopo Serengeti, Musoma na Dar es Salaam. 

Kwa sasa anaongoza makanisa mengi ndani na nje ya Tanzania. 

Gwajima ni mume wa mchungaji Grace ambaye amezaa naye watoto watatu ambao ni Ruth, Freeman na Manase.
Amefanikiwa kuhubiri katika nchi mbalimbali za Afrika, Marekani, Uingereza, Uswisi, Japan, Korea Kusini, Ujerumani, China na nyinginezo. 

Askofu huyo ambaye amejipatia sifa kutokana na staili yake anayodai kwamba anafufua wafu, alitangaza kupata Shahada ya Uzamivu (Phd) kutoka Chuo Kikuu cha Omega Global nchini Afrika Kusini na sherehe yake ilifanyika Hoteli ya Ubungo Plaza jijini Dar es Salaam.

KAKA YAKE AJITOKEZA
Methusela Gwajima, aliyejitambulisha kuwa ni mdogo wa Askofu Gwajima amejitokeza na kusema kuwa asili yao ni Kijiji cha Koromije Kwimba, Mwanza. 

Alisema kwa sasa familia ya mchungaji huyo ipo jijini Mwanza eneo la Mkolani ambako alisema yuko mama yake mzazi na baba yake yuko jijini Dar es Salaam kwa ajili ya matibabu. 

Akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam jana, Methusela alisema ingawa mdogo wake anaumwa, lakini anamtaka amwombe radhi Kardinali Pengo kwa njia alizozitumia kuwasilisha ujumbe wake wakati akimchafua.

MADAI YA KUTOROSHWA
Juzi, Kamanda wa Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Kamishna Suleiman Kova alitoa taarifa kwa vyombo vya habari akidai kukamata watu 15 wakitaka kumtorosha Askofu Gwajima. 

Kamanda Kova alidai watu hao walifika hospitalini saa 9:30 usiku kwa lengo hilo. 

Alisema walipekuliwa na kukutwa na begi ambalo lilikuwa na bastola aina ya Berreta yenye namba CAT5802 ikiwa na risasi tatu, risasi 17 za shotgun na vitabu viwili vya hundi za benki. 

Vitu vingine ni hati ya kusafiria yenye jina la Gwajima Josephat Mathias yenye namba AB 544809, kitabu cha hundi cha Benki ya Equity pamoja na nyaraka mbalimbali za Kampuni ya Puma, chaja ya simu, tablets, suti mbili na nguo za ndani.

GWAJIMA AIBUKA
Jana, Askofu Gwajima alivunja ukimya baada ya kukanusha taarifa za yeye kudaiwa kutaka kutoroshwa na wafuasi wake 15. 

Alisema bastola iliyokutwa katika begi lililochukuliwa wodini kwake, anaimiliki kihalali kwa ajili ya kujilinda na si vinginevyo. 

Akizungumza na waandishi wa habari wodini alikolazwa, Askofu Gwajima alisema ameshangazwa na taarifa zilizoandikwa katika vyombo vya habari kwamba wafuasi wake walitaka kumtorosha. 

“Juzi baada ya kupata taarifa zilizoandikwa kwenye mitandao ya kijamii kuwa nimefariki dunia, maaskofu wenzangu walikuja kuniona na kunishauri niachane na taarifa hizo huenda zilikuwa na lengo maalumu. 

“Baadaye nikawaambia wachungaji wangu waende nyumbani kwangu na kuchukua begi lililokuwa chumbani ambapo ndani yake palikuwa na baadhi ya nguo pamoja na bastola na nyaraka za umiliki wa silaha hiyo pamoja na vitu vingine. 

“Walifikisha begi na kuliweka hapa wodini nilikolazwa, lakini walitokea watu ambao walijitambulisha kuwa ni askari na kuomba mzigo ulioingizwa ndani na hapakuwa na ushindani nikawapa,” alisema Askofu Gwajima.

AZUNGUMZIA KUZIMIA KWAKE
Akizungumzia kuzimia kwake alipokuwa akihojiwa na polisi, alisema awali alitoa taarifa kwa askari hao kwamba alikuwa anaumwa kichwa, lakini hakusikilizwa wala kupatiwa huduma yoyote. 

Hata hivyo, alisema hana mgogoro wowote na Kardinali Pengo na kwamba kilichotokea alikuwa katika kazi yake ya kukemea.

TAARIFA MBILI ZA KAMANDA KOVA
Awali Kamishna Kova alisema bastola yenye namba CAT 5802 iliyokutwa kwenye begi la Askofu Gwajima haina umiliki wa mtu yeyote. 

Alisema kutokana na hali hiyo, Jeshi la Polisi linaendelea na uchunguzi ili kubaini kwanini Askofu Gwajima alikuwa akimiliki silaha kinyume cha sheria. 

Alisema wanasubiri atoke hospitali ili waendelee kumhoji zaidi. 

Baadaye jana jioni, Kova alituma taarifa nyingine kwa vyombo vya habari akisema uchunguzi wa kina na wa kitaalamu umethibitisha silaha hiyo inamilikiwa kihalali na Askofu Gwajima. 

Alisema risasi 17 za bunduki aina ya Shotgun yenye namba 102837 zinamilikiwa kihalali.

MAASKOFU KUMWONA IGP
Katika hatua nyingine, maaskofu na wachungaji kutoka makanisa ya Kipentekoste zaidi ya 100 leo wanatarajia kwenda kumwona Mkuu wa Jeshi la Polisi (IGP), Ernest Mangu ili kujadili suala la Askofu Gwajima. 

Akisoma tamko hilo kwa niaba ya wenzake, Askofu Damasi Mukassa kutoka Dodoma alisema wanakwenda kumwona IGP Mangu kwa ajili kuwataka watumie weledi na uadilifu kushughulikia suala hilo

VANESSA MDEE ATOBOA SIRI NZITO!!............soma hapa kujua alichokisema


VANESSA Mdee ambaye ameutambulisha rasmi wimbo wake mpya wa ‘No body but me’, ameweka wazi kwamba kushindwa kumudu gharama za uandaaji wa video, muziki bora kumekuwa sababu kubwa kwa wasanii wa kike kujiingiza katika mapenzi na watayarishaji wa muziki. 

Vanessa alitoa siri hiyo juzi alipotembelea ofisi za New Habari (2006) Ltd inayochapisha magazeti ya Mtanzania, Bingwa, Dimba, Rai na The African. 

Alisema wasanii wengi wa kike wanajikuta wanahitaji fedha kwa ajili ya kugharamia vitu vingi studio, video zao na gharama za mahitaji kwa ajili ya video bora lakini wanaposhindwa baadhi yao hujikuta wakinasa kimapenzi na maprodyuza ama watakaowagharamia. 

“Sijawahi kukutana na ushawishi wa kunitaka kimapenzi kwa sababu ninaweza kujigharamia kila kitu wakati ninapoandaa nyimbo zangu, lakini ni kweli wasanii wengi wa kike wasiokuwa na fedha ya kutosha wanajiingiza katika mapenzi baada ya kupungukiwa fedha,” alisema. 

Msanii huyo alisema alianza kujiandaa kuwa msanii mkubwa tangu akiwa shuleni kwa kujifunza kuimba, kucheza pamoja na kutumia vifaa vya muziki wakati familia yake ilipokuwa ikimuandalia vyanzo vya mapato kwa ajili ya muziki wake.

KUHUSU VURUGU KALI ZILIZOIBUKA MBEYA...........bofya hapa kuona mabomu yakilindima


KUNDI la vijana linalosadikiwa kuwa ni vibaka limeibuka na kufanya vurugu zilizoambatana na uvunjifu wa amani katika eneo la Soweto na Mwanjelwa jijini hapa. 

Kutokana na hali hiyo, Polisi mkoani Mbeya walilazimika kutumia nguvu ya ziada kuwatawanya vijana hao ambao tayari walianza kuweka matairi, mawe na magogo kwenye barabara kuu ya Dar es Salaam-Zambia katika eneo la Mwanjelwa. 

Kabla ya vurugu hizo baadhi ya wafanyabiashara ambao walikuwa kwenye mgomo wa kutokufungua maduka yao, wakishinikiza kuachiliwa kwa Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wafanyabiashara Tanzania Johson Minja, jana walitaka kufungua maduka yao kisha kuendelea na shughuli zao. 


Wakati, wafanyabiashara hao wakifungua maduka hayo, inasemekana baadhi ya wafanyabiashara ambao wao hawakuwa na utayari wa kufungua maduka, walianza kuwatisha wenzao ambao walitaka kufungua maduka yao. 

Mzozo huo ukiwa unaendelea baina ya wafanyabiashara hao, ndipo kundi la vijana, wanaodaiwa kuwa ni vibaka lilijitokeza na kuanza kufanya fujo zilizoambatana na uvunjifu wa amani. 

Wakizungumza na Mtanzania kwa nyakati tofauti katika eneo la tukio, baadhi ya wafanyabiashara hao, walisema kuwa, wao wameamua kufungua maduka yao baada ya kupata taarifa kutoka kwa wenzao wa mikoa ya jirani kama vile Iringa, Njombe na Ruvuma kwamba wanaendelea na shughuli zao za uuzaji wa bidhaa kama kawaida. 

“Mikoa mingine tayari wafanyabiashara wenzetu wanaendelea na shughuli zao hivyo baada ya kusikia hivyo na sisi leo tumeamua kuja kufungua biashara nzetu, lakini tunashangazwa na hawa wanaofika na kututisha,”alisema mfanyabiashara Edwin Sanga wa Mwanjelwa. 

Akizungumzia vurugu hizo Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Mbeya, Ahmed Msangi, alithibitisha kutokea kwa tukio hilo lakini alikanusha madai ya kwamba askari walitumia mabomu katika kutuliza ghasia hizo. 

“Tukio hili la uvunjifu wa amani lilitaka kutokea lakini vijana wangu hawajatumia mabomu, silaha wala nguvu ya aina yoyote katika kurudisha hali ya amani, zaidi walichokifanya askari ni kufanya doria katika maeneo hayo ambayo tayari yalionyesha viashiria vya kutokea kwa vurugu,” alisema. 

Alisema, wakati gari hizo za doria zikipita kwenye eneo hilo la tukio na kuweka ulinzi kwenye eneo ambalo tayari vijana waliweka matairi barabarani, wahusika walianza kukimbia wenyewe na mpaka sasa hakuna mtu aliyekamatwa kutokana na vurugu hizo

Gwajima Afunguka......Asema Aliagiza Bastola yake ili Ajihami Baada ya Taarifa Kuzagaa Mitandaoni kuwa Amefariki Dunia


Hii ni Picha iliyosambazwa katika mitandao ya kijamii ikidai kuwa Gwajima kafariki dunia na yuko Mochwari.Taarifa hizi zilimpa hofu Gwajima na kumfanya Aagize Bastola yake kwa ajili ya kujihami.

**********Utata umeibuka kuhusu bastola waliyodaiwa kukamatwa nayo wafuasi wa Kiongozi wa Kanisa la Ufufuo na Uzima, Askofu Josephat Gwajima baada ya kiongozi huyo kusema anaimiliki kihalali kinyume na maelezo ya polisi.


Gwajima aliyetolewa kwenye chumba cha uangalizi maalumu cha Hospitali ya TMJ jana, amelitaka Jeshi la Polisi kurudisha bastola hiyo, akisema ni mali yake na aliiagiza ipelekwe hospitalini kwa sababu ya kujilinda.

Akizungumza na waandishi wa habari hospitalini hapo alipolazwa baada ya kuishiwa nguvu na kupoteza fahamu akiwa katika mahojiano na polisi, Gwajima alisema anashangaa kukamatwa kwa wachungaji wake waliokuwapo kwa ajili ya kumlinda.

Hata hivyo, katika kwa upande mwingine, Kamanda wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Suleiman Kova alisema bunduki hiyo haina umiliki halali wa Gwajima wala wa wachungaji 15 waliokamatwa lakini baadaye jioni baada ya maelezo ya Gwajima, alitoa taarifa akisema bastola hiyo ni mali halali ya askofu huyo. Pia alisema kuhusu risasi 17 za bunduki aina ya Shortgun, Gwajima anamiliki bunduki ya aina hiyo lakini akasema uchunguzi kuhusu watu hao 15 unaendelea.

Kauli ya Gwajima Akizungumza kwa shida akiwa amejishika tumbo, Gwajima alisemaalipopata taarifa za uvumi kwenye mitandao ya kijamii kuwa amefariki dunia, aliagiza wachungaji waende hospitalini kwa ajili ya kumlinda, lakini wakaishia mikononi mwa polisi wakidaiwa kutaka kumtorosha.

Alisema alihofia kuwapo kwa watu wabaya ambao wangeweza kumdhuru halafu wakasingizia kitendo hicho kufanywa na polisi kwa kuwa alipata tatizo akiwa mikononi mwao.

“Usiku wasiwasi ulizidi, huku kila mmoja akiwa hafahamu kwa nini ujumbe wa namna ile unasambazwa kwenye mitandao, msambazaji ni nani, ana nia gani, nikaamua kuwaagiza waniletee silaha yangu iliyokuwa kwenye begi ili likitokea lolote niweze kujilinda,” alisema Gwajima.

Alisema alishangaa kukamatwa wachungaji wake na kuchukua silaha iliyokuwa ndani ya begi na hadi jana hakuwa ameulizwa chochote kuhusu umiliki wa silaha hiyo.

“Kabla sijazungumza na waandishi kueleza ukweli wa kinachodaiwa kuwa nilitaka kutoroshwa na wachungaji wangu, nilitaka kuzungumza na ZCO (Mkuu wa Upelelezi Kanda Maalumu), lakini hajaja, kadi ya ile silaha ninayo,” alisema Gwajima.

Alisema madai kuwa alitaka kutoroka ilihali polisi alikwenda mwenyewe akitokea Arusha baada ya kusoma katika vyombo vya habari kuwa anatafutwa.

Alifafanua kuwa hata alipofika polisi kwa ajili ya mahojiano hakuwa na shaka hata kidogo, lakini alishangaa kuona anaishiwa nguvu kila baada ya muda na alipoona kichwa kinamuuma, akawaomba wampeleke hospitali ili mambo mengine yafuate baadaye, kitu ambacho hakikufanyika kwa wakati.

Wasiwasi kwa polisi
Alisema alijaribu kuomba apelekwe hospitali mara kadhaa, lakini hakuna aliyekubaliana naye hadi alipopoteza fahamu na kupelekwa hospitali ya Polisi Kurasini.

“Hivi hata kama ni chombo cha usalama, nimepata matatizo nipo mikononi mwao, halafu nikubali kutibiwa katika hospitali yao, sikulitaka hilo na hata waliposema nikatibiwe Muhimbili pia sikutaka, ndiyo maana nilikuja hapa, sisemi moja kwa moja kama Polisi wanahusika lakini kuna vitu vinanitia shaka,” alisema Gwajima.

Alieleza kuwa anatilia shaka Jeshi la Polisi kutokana na kuwapo vitu vingi vinavyoashiria wana kitu kingine wanatafuta, kwani jana tulikuwa na hofu ya kuvamiwa, waliokuja kutuvamia ni wao, sikugombana na Pengo, nilikuwa namkemea kama kiongozi mwenzangu wa kiroho wao, wameligeuza ni kesi.

“Sijawahi kulitilia shaka Jeshi la Polisi lakini katika hili napata wasiwasi mwingi, sina ugomvi na Kardinali Pengo, nampenda, hajanilaumu, wala kunishtaki, nilikuwa namkemea katika masuala yetu ya mabaraza ya dini na siyo vinginevyo,” alisema Gwajima.

Gwajima pia alionyesha wasiwasi wake kwa kile kilichokuwa kinang’ang’aniwa na polisi kwenda kupekua nyumbani kwake kuwa hakikuwa kitu kizuri.

Kova alipinga
Wakati Gwajima akisema hayo, Kamanda wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Suleiman Kova alisema bastola waliyokutwa nayo wafuasi wa Gwajima haimilikiwi kihalali.

“Tumegundua kuwa katika wale watu waliokuwa pale akiwamo Gwajima mwenyewe, (bastola) haikuwa katika umiliki wao halali, kwa hiyo hapa kuna kesi ya kupatikana na silaha bila kibali.”

Akizungumzia tuhuma kwamba polisi walimpekua mke wa Gwajima, Kova alisema hakuna polisi waliofika nyumbani kwake kufanya upekuzi wowote na kama wakitaka kufanya hivyo watafuata taratibu maalumu za upekuzi.

Akijibu swali kuhusu mahali Gwajima alipotakiwa kutoroshewa, Kova alisema uchunguzi huo bado unaendelea na utakapomalizika wahusika watafikishwa mahakamani.

Pia alipoulizwa kama Mwadhama Polycarp Kardinali Pengo amemsamehe Gwajima, kwani polisi imng’ang’anie, Kova alisema;“amesema anamsamehe lakini haingilii mambo ya sheria.”

Kuhusu sababu za Gwajima kuzimia wakati akihojiwa, Kova alisema anayepaswa kuulizwa kwa nini alianguka wakati akihojiwa na polisi ni Gwajima mwenyewe.

“Siri za mahojiano huwa hazitolewi kabla ya ushahidi mahakamani, sababu ya kupata shock (mshtuko) atajua mwenyewe, kwa kuwa ukifanyiwa jambo ukafurahi au ukachukia wewe ndiyo unajua ilikuwaje, chochote kitakachotokea ukicheka, ukinuna, ukizimia, wewe ndiyo tukuulize ilikuwaje mpaka ukazimia kwa sababu hisia unazipata wewe,”alisema Kova.



Makonda amtembelea
Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Paul Makonda ambaye alikuwa amemwandikia Gwajima barua akimwita ofisi kwake, jana mchana alimtembelea hospitalini hapo kwa ajili ya kumjulia hali kiongozi huyo lakini akasisitiza kuwa nia yake bado ipo palepale.

“Nilimtaka leo aripoti ofisini kwangu lakini kwa bahati mbaya anaugua na amelazwa. Nitakwenda kumuona ili nijue hali yake ikoje,” alisema Makonda kabla ya kufunga safari kwenda hospitali alikolazwa.

Alisema pia atataka kiongozi huyo wa kiroho amweleze anavyoelewa maana ya uhuru wa kuabudu unaoelezwa katika Katiba, usajili wa taasisi yake na katiba ya taasisi hiyo.

“Mimi ni mwenyekiti wa Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Wilaya ya Kinondoni. Niliagiza polisi wamkamate na baadaye wakimaliza kumhoji aje kwangu pia atahojiwa na jopo la watu 20,” alisema Makonda.

Baada ya Kuhamia Nyumba Mpya, Diamond na Zari Roho Mkononi, Yabainiki Kwake ulinzi ni Sifuri, Mwenyewe Akiri Kuishi kwa Hofu

TAHADHARI ichukuliwe! Habari zikufikie kuwa, baada ya staa mkubwa wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz‘ na mpenzi wake, Zarinah Hassani ‘Zari’, kuhamia kwenye mjengo wake mpya uliopo Madale jijini Dar, imebainika kuwa familia hiyo inaishi roho mkononi kufuatia ulinzi sifuri, jambo linalowafanya kuishi kwa hofu tupu

Kikizungumza kwa hofu juu ya familia hiyo, chanzo chetu makini kilipasha kwamba, pamoja na Diamond kutumia mamilioni ya fedha kujenga nyumba hiyo ya gharama kubwa, sasa changamoto imehamia kwenye ulinzi na usalama wao

“Jamani watu wanampongeza Diamond kwa kuhamia nyumba mpya lakini wale jamaa aisee wanapaswa kuombewa kila kukicha.

“Pamoja na kushusha mjengo wa maana bado changamoto ni juu ya ulinzi wao.

“Huwezi kuamini Diamond bado anaishi kizamani sana na sijui kwa nini anajiamini kiasi hicho wakati anajua wazi kuwa yeye ni staa wa Afrika na hapaswi kuishi kwa ulinzi hafifu.

MAENEO HATARISHI?

“Nasema hivi kwa sababu hata maeneo anayoishi ni hatari sana kwake hivyo anatakiwa kuwa na ulinzi mkali ili tu siku moja asije akafanyiwa kitu ambacho taifa likaingia kwenye hasara ya kumpoteza nyota mkubwa kama yeye.

“Nina uhakika asilimia mia moja Diamond hadi leo hajaanza hata kufanya process (taratibu) za kuchukua silaha (bastola).

“Mimi naijua vizuri Madale ni sehemu ambayo watu huwa wanavamiwa mara kwa mara na wanaishi kwa hofu kama Diamond anavyoishi.

HIKI NDICHO KINACHOMPONZA

“Kitu kingine kinachomponza Diamond ni ishu ya kuweka kila kitu kilichopo ndani kwake mitandaoni. Usione kila mtu anasifia lakini kuna wengine wanavitolea macho.

“Kwa mfano katupia picha za toilet (choo) ambacho kimepakwa dhahabu na kusema kimegharimu shilingi milioni 70.

“Hajakaa sawa akatupia picha za jikoni kwake kuna vitu vingi vya thamani kubwa kila mahali mpaka kwenye korido kuna flat screen (runinga). Huko si ni kuwakejeli watoto wa mbwa? Ni vizuri akaacha kufanya hivyo kwa sababu anawapa watu tamaa,” kilitiririka chanzo hicho.

ANA ULINZI GANI?

Juu ya ulinzi wa nyumbani kwa Diamond, chanzo hicho kilidai kwamba, mbali na baunsa anayewalinda aitwaye Mwarabu hakuna askari wa silaha anayelinda nyumbani hapo hivyo jamaa anatakiwa kufanya haraka kuajiri walinzi wenye silaha.


Baada ya habari hizo na uchunguzi wa kutosha, Ijumaa Wikienda lilimsaka Diamond a.k.a Dangote au Chibu ili kujua namna anavyoishi na jinsi anavyoimarisha ulinzi wake na familia kwa jumla.

Diamond, mbali na kukiri kuwa na hofu, alikuwa na haya ya kusema: “Suala la ulinzi wangu nalijua mwenyewe lakini zaidi watu wanatakiwa kujua mimi nipo na mlinzi na ninaendelea kuimarisha ulinzi wa nyumbani kwangu.

“Sidhani pia kama ni suala zuri sana kwa watu kujua siri za ulinzi wangu ila mambo mengi ya kujilinda niko kwenye michakato ya mwisho kukamilisha na soon (haraka) mambo yote yatakaa levo maana huwezi ukafanya kila jambo kwa wakati mmoja,” alisema Diamond huku akikubaliana na ushauri wa gazeti hili juu ya kuongeza ulinzi alionao wa baunsa.

ILIWAHI KUMTOKEA SUGU

Huko nyuma iliwahi kumtokea Mwanamuziki Joseph Mbilinyi ‘Sugu’ ambaye kwa sasa ni Mbunge wa Mbeya Mjini (Chadema) ambapo alikuwa amerejea kutoka nchini Uingereza.

Akiwa amepanga nyumba nzima maeneo ya Tegeta, Dar, Sugu alifanyiwa makala ya runingani na kuonesha vitu vya thamani vya nyumbani kwake.

Siku chache baada ya kipindi hicho kuruka runingani, jamaa huyo alivamiwa na kuporwa kila kitu lakini yeye hakudhurika.

Video ya Davido akimponda Diamond, wikii hii alipokua Kenya.............bofya hapa kuona video hiyo


Inaonekana bifu la Davido na Diamond bado linaendelea japo wao wenyewe kusema kua hakuna bifu kati yao wawili. Wiki hii Davido alikua Kenya na kibaya zaidi alilalamikiwa na mashabiki wake kua alipanda stejini kalewa na kufanya show iliyochukua dakika 20 tu kisha akashuka. 


Kabla ya Show hiyo Davido alifanyiwa mahojiano na kituo cha Tv cha Kenya na Davido aliulizwa swali kama nyimbo za Davido zinapigwa nchini Nigeria alisema NO akimaanisha kua hua nyimbo za Diamond hazipigwi Nigeria. Ila alisema nyimbo za wasanii wengine wa Afrika Mashariki zinapigwa kama za Saut Soul. 


Unaweza tazama video ya Davido alipokua akihojiwa hapa chini.

Tamko la Maaskofu kuhusu sakata la Gwajima............soma hapa


Baadhi ya Maaskofu wakifuatilia kwa makini tamko lililokuwa linatolewa na wenzao ambao hawapo pichani.

Maaskofu kutoka madhehebu mbali mbali ya Kikristo nchini Tanzania wanakusudia kuonana na mkuu wa jeshi la polisi IGP Ernest Mangu, ili kupata suluhu kuhusu sakata linalomkabili mkuu wa kanisa la ufufuo na uzima, askofu Josephat Gwajima.

Aidha, maaskofu hao pia wameonyesha masikitiko ya kile walichodai kuwa ni vituo vya polisi kutoonekana kuwa ni mahali salama kwa watuhumiwa wa makosa mbali mbali wanaofikishwa hapo. 

Askofu Gwajima amelazwa katima hospitali ya TMJ jijini Dar es Salaam, alikopelekwa kwa matibabu baada ya kuanguka na kupoteza fahamu wakati akihojiwa na polisi, kwa tuhuma za kumkashifu askofu wa kanisa katoliki jimbo kuu la Dar es Salaam, Muadhama Kadinali Polycarp Pengo.

Wakizungumza katika mkutano wa pamoja waliouitisha jijini Dar es Salaam leo, maaskofu hso kupitia kwa msemaji wao Damas Mukassa wamesema inasikitisha kuona kuwa mchungaji Gwajima alijisalimisha polisi akiwa mzima na afya njema lakini ghafla akapoteza fahamu na afya yake kuwa mashakani kwa sababu ambazo hazijajulikana.

Katika tamko hilo ambalo linaashiria kutoridhishwa na namna sakata la askofu Gwajima linavyoshughulikiwa, maaskofu hao wameshangazwa na kupinga vikali madai ya polisi kwamba kulikuwa na njama za kumtorosha kiongozi huyo wa kidini ambae katika siku za hivi karibuni habari zake zimekuwa zikipamba vyombo mbali mbali vya habari.

Kwa mijibu wa tamko hilo, njama za kumtorosha askofu Gwajima hazina ukweli wowote ikizingatiwa kiwa alikwenda polisi kwa hiari yake mwenyewe pasipo kushurutishwa na mtu yoyote. 

Aidha, imedaiwa pia kuwa hata watu kumi na tano wanaotuhumiwa kuratibu njama za kumtorosha kiongozi huyo ni wafuasi wake wa karibu na ambao aliambatana nao siku ya ijumaa alipojisalimisha kituo cha polisi cha kati, yalipo makao makuu ya polisi kanda maalumu ya Dar es Salaam.

Kwahiyo katika kuhitimisha tamko lao, maaskofu hao wameazimia kumshauri IGP Mangu aangalie uwezekano wa kuacha swala la Gwajima limalizwe kwa njia na taratibu zinazosimamia imani ya dini ya Kikristo.

Ina sikitisha sana:Mwanamume anywa sumu baada ya kumchoma kisu mkewake


MWANAMKE mmoja mwenye asili ya Kiarabu, Salma Amuri (39) (pichani) mkazi wa Mji Mpya, Kawe jijini Dar, amenusurika kifo baada ya kuchomwa visu sehemu mbalimbali za mwili wake ikiwemo tumboni na mumewe aliyetambulika kwa jina moja la Selemani.Mwanaume huyo naye baada ya tukio hilo alijaribu kujiua kwa kunywa sumu, chanzo kikidaiwa kuwa ni wivu wa mapenzi. 


Salma Amuri anayedaiwa kuchomwa visu na mumewe akiwa hoi hospitalini.

Kwa mujibu wa taarifa kutoka kwa chanzo chetu, tukio hilo lilitokea saa saba usiku wa kuamkia Alhamisi iliyopita ambapo mwanamke huyo alijeruhiwa vibaya kiasi cha kufanya utumbo wake kutoka nje, kabla ya ndugu na wasamaria wema kuwachukua wawili hao na kuwakimbiza Hospitali ya Mwananyamala, wote wakiwa mahututi.

Gazeti hili lilizungumza na mwanamke huyo hospitali ambapo alieleza kisa cha tukio hilo.

“Migogoro ndani ya ndoa yetu tuliyofunga miaka ishirini iliyopita na kufanikiwa kupata watoto na wajukuu, ilianza tangu Novemba, mwaka jana baada ya kutembelewa na ndugu yangu aliyekuja Tanzania akitokea Saudi Arabia anakoishi.

“Mume wangu alikuwa ananishutumu kwamba ameambiwa na majirani mimi natembea na huyo mtoto wa mama yangu mdogo, jambo ambalo siyo la kweli kwani hata kiumri, ni mdogo, hajafikisha hata miaka thelathini,” alisema mwanamke huyo.



Moja ya jeraha alolipata mwilini mwake.

“Usiku siku ya tukio saa saba usiku alirudi nyumbani akawa amekaa sebuleni lakini baada ya kumtaka twende tukalale aligoma, mimi nikarudi ndani, mara akaja na kuniambia ameamua kujiua huku akinionesha sumu aliyokuwa ameiandaa kwenye chupa ili anywe.”Aliongeza kuwa alivamiwa ghafla na kushambuliwa kwa kisu kisha alipoteza fahamu akajishitukia akiwa pale hospitali.

Jitihada za kumsikia mumewe ambaye awali naye alikuwa amelazwa kwenye hospitali hiyo, ziligonga mwamba kwa kuwa alikuwa amelazwa chini ya ulinzi wa polisi.Kamanda wa Polisi Kanda ya Kinondoni, jijini Dar, ACP Camillius Wambura alikiri kutokea kwa tukio hilo. “Mumewe alihamishiwa Hospitali ya Taifa ya Muhimbili kutokana na hali yake kuwa mbaya na mwanamke yupo Mwananyamala, uchunguzi bado unaendelea,” alisema Wambura.
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...